Wanachama
wa Simba wakinyoosha mikono kupinga uongozi uliopo madarakani wakati wa
mkutano wao jana katika ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam..
Release No. 049b
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 18, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 18, 2013
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua kutoka
uongozi wa Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa
kuwa wanachama wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es
Salaam.
Vilevile katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.
Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.
Hata hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na kanuni zilizopo.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:
Post a Comment