EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, March 16, 2013

UKIJIRAHISI KWA WANAUME, WATAKUPITIA NA KUKUACHIA SHOMBO...

MAPENZI ni furaha, lakini siyo wote hubahatika kuwa katika furaha hiyo. Makosa fulani yakifanyika, ama kwa kujua au kwa bahati mbaya basi ndiyo mwanzo wa kupoteza furaha katika mapenzi.
Kwa bahati mbaya sana, baada ya kupoteza furaha, ni vigumu kuirudisha kwa haraka, hata kama ulikuwa na mwenzi mwingine kwa muda mrefu lakini baada ya kugundua matatizo yake na kuachana naye, utapata shida sana kupata mbadala.
 
Lakini pia, hata kama utampata ni vigumu sana kumzoea kwa muda mfupi, kuzoea mazingira na kujihakikishia kuwa ndiye mwenzi wako wa kudumu.
 Siyo ajabu sana wapenzi kuachana, lakini inapotokea wewe unakuwa wa kuachwa kila siku, lazima ujue kwamba kuna tatizo, tena tatizo lenyewe lazima litakuwa upande wako.
Ni jambo gumu kidogo kupata hekima ya kugundua jambo hili, lakini waliobahatika kupata wamekuwa wakifanya maamuzi ambayo hayawaumizi mioyo yao.
 
Haya mambo yanawezekana rafiki zangu. Kwanza ni kukubali kujifunza, kuangalia wapi ulikosea, ni kipindi gani wenzi unaoachana nao wanapatwa zaidi na hisia za kukuacha n.k. Baada ya hapo ni rahisi kusogea mbele zaidi katika kujua jinsi ya kutatua tatizo ulilonalo. Katika mada hii nazungumza zaidi na dada zangu.
Wapo wanawake wengi sana ambao wanahangaika kwa sababu ya kuachwa kila siku. Kila mwanaume anayekuwa naye, baada ya muda mfupi tu, anaachana naye!
Hajui tatizo, badala yake anaishia kulia tu. Kulia kwako hakutakusaidia lolote kama hutakaa chini na kujiuliza ni wapi kwenye matatizo, ni sehemu gani huwa unakosea!

Kujua chanzo cha tatizo ni mwanzo mzuri sana wa kuelekea kwenye kupata ufumbuzi. Una miaka ishirini na nne tu, lakini umeshakuwa na wanaume tisa! Hili ni tatizo, tena kubwa linalohitaji dawa ya kuponya na siyo ya kutuliza maumivu.
Sikia kilio cha dada huyu: “Mpaka sasa nimechoka, nahisi kama sitakiwi kuwa na mpenzi, maana kila ninayekuwa naye lazima ananiacha. Neno nakupenda halina thamani kabisa katika maisha yangu ya sasa, yaani nimechanganyikiwa kabisa kaka Shaluwa. Utanisaidiaje niweze kupenda tena?”
 
Hayo ni maneno ya dada Zulfa wa Sinza jijini Dar es Salaam, ambaye alipata kuzungumza nami ofisini kwangu hivi karibuni.
Kilio kama cha Zulfa kipo kwa wanawake wengi sana nchini. Zulfa aliondoka akiwa mpya baada ya kuzungumza naye kwa takriban saa mbili. Niliongea naye mambo mengi sana, ambayo siwezi kuyaandika yote hapa, lakini kwa uchache sana pitia vipengele vifuatavyo;

UNAJIRAHISISHA?
Kwanza jaribu kujichunguza kama una tabia ya kujirahisisha. Ni kweli umekuwa na tabia ya kujishusha thamani na kuona kama wewe ni wa kuonewa, kuchezewa? Mwanaume mwenye ndoto na mwanamke wa baadaye wa maisha yake (mke) hahitaji mwanamke wa aina hii. Anapenda zaidi awe na mwanamke mwenye msimamo anayetambua thamani yake yeye mwenyewe na maisha yake kwa ujumla. Hapendi mwanamke ‘maharage ya mbeya’ maji mara moja!
 
Kama utakuwa wa aina hii, hata kama atakuwa amekupenda, ataishia kukutumia na kukuacha, kwani wewe mwenyewe umejionesha wa namna hiyo.
Mwanaume anapenda sana mwanamke wa kumsumbua kidogo, angalau baadaye apate stori za kusema; ‘lakini mama nanilii ulinisumbua!’ Huu ni ukweli ambao baadhi ya watu wanaukwepa. Acha kujirahisisha.
Kujirahisisha huku ni pamoja na suala zima la kufanya mapenzi, usiwe na haraka na tendo hilo, usiulizie juu ya kufanya mapenzi, lakini kama ikitokea jamaa akataka, usikubali haraka. Onyesha msimamo wako, ukiainisha usivyotaka kuchezewa.

CHUNGUZA MIENENDO YAKO...
Wakati mwingine mambo yako yasiyotamanika yanaweza kuwa chanzo cha wewe kuachwa na wenzi wako kila wakati. Angalia tabia zako, tizama mienendo yako, marafiki zako, kauli zako na kila kitu ambacho unadhani kinaweza kuwa tatizo.
Mwanaume hapendi kuwa na mwanamke ambaye ana kampani mbaya, kwani anaamini na wewe pia inawezekana ukawa na tabia chafu kama rafiki zako, lakini kauli nzuri kwa mwenzi pia ni kati ya mambo ambayo mwanaume mwenye nia ya kuoa atavutiwa navyo. Jiangalie upya!
Itaendelea wiki ijayo

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate