Chadema inadai wapandaji wa mbegu ya udini ni CCM
Moshi. Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kimesema iwapo amani itatoweka kutokana na vurugu
za kidini, watawashtaki viongozi wa CCM Mahakama ya Kimataifa ya The
Heague.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita
na Mwenyekiti wa Chadema Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael wakati
akimkaribisha Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo kuhutubia
mkutano wa hadhara.
Michael ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Moshi,
alisema baadhi ya viongozi wa Serikali ya CCM ndiyo kiini cha mbegu za
chuki za kidini, walipoituhumu Chadema kuwa ni chama cha kidini.
“Nataka niwaambie leo, amani ya Tanzania
ikivurugika tunawapeleka viongozi wote wa Serikali ya CCM The Heague,
wao ndiyo chanzo cha chuki hizi za udini ambazo zinaligawanya taifa,”
alisema Michael.
No comments:
Post a Comment