Zaidi
ya asilimia saba ya watanzania wanakabiliwa na ugonjwa wa kisukari
ambapo idadi hiyo imekuwa ikiongezeka zaidi kwa siku za karibuni kutoka
na kubadilika kwa mfumo wa maisha na ulaji.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. HUSSEIN MWINYI amesema idadi kubwa ya wagonjwa wa kisukari wapo mijini na kubainisha kuwa kutokuwepo kwa utamaduni wa kupima afya mara kwa mara pia kunachangia athari kubwa za ugonjwa wa kisukari.
Akizindua gari la kutolea huduma kwa wagonjwa wa kisukari lililotolewa na mashirika yanayoshughulikia wagonjwa wa kisukari nchini Denmark ambalo litakwenda kufanya kazi Kanda ya Ziwa Dk. MWINYI amesema kwa siku za karibuni kumekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wenye maradhi yasiyoambukizwa.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo kisukari Dk. ALY MZIGE amewataka watu wanaopatikana na kisukari kuzingatia masharti ya ulaji na ufanyaji wa mazoezi.
Uzinduzi huo pia umehudhuriwa na wanachama wa chama cha kisukari nchini ambapo mwenyekiti wa chama hicho Prof. ANDREW SWAI na ZAHORO MWENYEWE ambaye ni mwanachama wamewataka wananchi kutosikiliza maneno ya mitaani kuhusu ugonjwa wa kisukari na kupima afya zao.

No comments:
Post a Comment