Matukio ya majengo kuporomoka nchini
Bangladesh ni ya kawaida kutokana na majengo mengi marefu kujengwa kinyume na
sheria za ujenzi.
Jengo lililoporomoka lilikuwa na kiwanda cha nguo, benki na maduka kadhaa. Liliporomoka asubuhi wakati watu wakielekea makazini.
Jengo lililoporomoka lilikuwa na kiwanda cha nguo, benki na maduka kadhaa. Liliporomoka asubuhi wakati watu wakielekea makazini.
Watu wengi walikusanyika karibu na eneo la tukio wakiwatafuta ndugu na marafiki. Haijafahamika kilichosababisha jengo hilo kuporomoka, lakini vyombo vya habari nchini humo vimesema kwamba, nyufa zilionekana kwenye jengo hilo siku ya Jumanne.
Polisi wameviambia vyombo vya habari
kwamba, waliona ghafla sehemu ya nyuma ya jengo hilo ikianguka Jumatano asubuhi
na baada ya muda mfupi jengo lote likafuatia isipokua nguzo kuu na sehemu ya
ukuta wa mbele hali iliyosababisha taharuki.
Maafisa wanasema, ni sehemu ya chini
pekee ya jengo hilo la Rana Plaza ndio ilibakia imara baada ya kuporomoka,
wakati wanajeshi na waokoaji wa idara ya zimamoto wakiwa na vifaa vya kukatia
vyuma na matingatinga wakifukua vifusi ili kuwaokoa watu walionaswa .
Mkuu wa polisi wa eneo hilo,
Mohammed Asaduzzaman, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, hali ilikua
mbaya sana.
No comments:
Post a Comment