STAA kiwango wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amenaswa kwenye kaburi
la marehemu Steven Kanumba peke yake baada ya watu wote kuondoka.
Aunt Ezekiel
STAA kiwango wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amenaswa kwenye kaburi
la marehemu Steven Kanumba peke yake baada ya watu wote kuondoka.
Tukio hilo lilitokea juzikati katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar
ambapo tofauti na wasanii wengine waliofika kumuenzi marehemu aliyekuwa
akitimiza mwaka mmoja kaburini, Aunt alibaki peke yake, akapiga magoti
kaburini na kuanza kulia kwa uchungu.
Wadau mbalimbali
waliohudhuria katika makaburi hayo, walishangazwa na tukio la Aunt kukaa
makaburini kwa takribani dakika kumi huku wengine wakimuonea huruma
kutokana na msanii huyo kushindwa kuzuia hisia zake.
“Kiukweli kila
nikifika katika kaburi la Kanumba lazima nihisi kuchanganyikiwa. Kuna
wakati mwingine siamini kabisa kama huyu mtu hatunaye tena hivyo
nahitaji kubaki hata peke yangu kaburini nimsalie kisha niondoke,”
alisema Aunt huku akifuta machozi.
No comments:
Post a Comment