EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, April 16, 2013

Bunge aibu tupu - NKAMIA AOMBA MSAMAHA.

*Wabunge waporomosha matusi hadharani

Naibu Spika Job Ndugai
TABIA ya wabunge kurushiana matusi wakati wa mjadala wa Bunge, imezidi kushika kasi, baada ya tabia hiyo kuendelea tena jana wakati wa mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2012/13.

Pamoja na tabia hiyo kuendelea tena jana, wiki iliyopita Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu (CHADEMA), alisema Baraza la Mawaziri linaundwa na mawaziri wapumbavu. Kwa siku ya jana, tabia hiyo ilianzia kwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kisha ikasisitizwa na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM).

Wakati Nkamia akichangia bajeti hiyo na kueleza jinsi asivyokubaliana na vitendo vya udini vinavyodaiwa kuwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Sugu aliingilia kati bila kuruhusiwa na kusema, je Lwakatare.

Baada ya Sugu kusema neno hilo, Nkamia alikatisha kuchangia na akasema:

“Sugu naomba unyamaze mimi ndiye nazungumza, mimi siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa,” alisikika Nkamia.MACHALI AOMBA MWONGOZO
Nkamia aliposema hivyo, wabunge waliguna na Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisimama na kuomba Mwongozo wa Spika akitumia Kanuni ya 64 (1g) inayozuia wabunge kutumia lugha zisizofaa.
Kwa mujibu wa Machali, kauli ya Nkamia ilionyesha kuwa, mbwa ni wabunge wanaosikiliza mjadala na mwenye mbwa ni Naibu Spika ambaye wakati huo, alikuwa akiliongoza Bunge.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja mbunge mwenzake huyo kufuta kauli yake, kwa kuwa ilikuwa inakiuka Kanuni za Bunge.

NKAMIA AENDELEA KUCHANGIA

Hata hivyo, Nkamia alisema hawezi kukubaliana na alichosema Machali kwa kuwa alichokisema hakikuwa matusi bali tafsiri ilivyofanywa na Machali haikuwa sahihi.

“Siwezi kukubaliana na kauli ya mdogo wangu Machali, nilichokisema siyo tusi, bali ni kutojua namna ya kutafsiri maneno. Kama hoja hiyo ingekuwa imetolewa na mtu makini, ningemuelewa, lakini kwa kuwa ni Machali, siwezi kuichukua,” alisema Nkamia na kuendelea kuchangia.
 KAULI ZA LUSINDE
Wakati Nkamia akisema hayo, awali Lusinde naye alimkashifu Mbunge wa Nyamagana, Hezekiah Wenje (CHADEMA), baada ya kumwambia kuwa hajui kinachomuwasha.

Kabla ya kutoa kauli hiyo, Lusinde alisema kuna chama kimoja cha siasa ambacho kimekuwa kikipewa fedha na wafadhili wa nje na kwamba fedha hizo zinatumiwa vibaya kwa kuivuruga nchi.

Kwa mujibu wa Lusinde, chama hicho kimepewa fedha hivi karibuni na wakati wa makabidhiano hayo wananchi wengi waliona.
LUSINDE AENDELEA
Wenje alipomaliza kutoa taarifa yake, Lusinde alisimama tena na kusema katika mazungumzo yake hajaitaja Chadema, bali alisema kuna chama kimoja cha siasa.

“Siwezi kuikubali taarifa hiyo na nadhani huyu mtu bado amechanganyikiwa na uchaguzi wa Kenya, mimi sijaitaja Chadema bali nimesema kuna chama kimoja cha siasa na CCM pia ni chama cha siasa, sijui yeye anawashwa nini,” alisema Lusinde.

Pamoja na hayo, Lusinde alisema anawashangaa baadhi ya wabunge wanaochochea vurugu nchini na kusema kuwa vurugu zikitokea hakuna atakayesalimika.

“Kuna watu hapa wanachochea vurugu na sijui zikitokea wao watajificha wapi, mimi mtoto wangu wa mwisho ana miaka minane na mtoto wa Dk. Slaa sijui ana wiki ngapi.

“Nawashangaa wabunge wengine wanasema eti walemavu wanapewa mimba zisizotarajiwa, wakati hata hapa bungeni kuna wabunge wana mimba zisizotarajiwa na ipo siku tutawataja,” alisema.MAGDALENA SAKAYA
Kauli hiyo, ilionekana kumkera Mbunge wa Viti Maalum, Magdalena Sakaya (CUF), ambaye aliomba mwongozo wa Spika akitaka Lusinde alieleze Bunge ni mbunge gani amepata mimba bila kutarajia.

Kwa mujibu wa Sakaya, kauli ya Lusinde ilionekana kuwakashfu wabunge ambao licha ya umri wao mkubwa inaonekana wapo wanaobeba mimba zisizotarajiwa, jambo ambalo alisema ni kuwadhalilisha.NAIBU SPIKA AFAFANUA
Akizungumzia kauli zisizofaa, Naibu Spika aliwataka wabunge wawe makini na kauli zao kwani Bunge linaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni.

Pamoja na hayo, alisema Sakaya ambaye alikuwa ameomba mwongozo juu ya wabunge kupata mimba zisizotarajiwa, alifuta mwongozo huo kutokana na sababu anazozijua yeye.NKAMIA AOMBA MSAMAHA
Kutokana na uzito wa maneno yaliyokuwa yametolewa na Nkamia, Spika wa Bunge alipokuwa akijiandaa kuahirisha Bunge hadi jana jioni, alimtaka Nkamia azungumzie kauli ya kutotaka kuzungumza na mbwa.

Alipokuwa akitoa ufafanuzi, Nkamia alimwomba radhi Sugu na kusema kuwa aliyasema maneno hayo kwa sababu alikerwa na kauli iliyotolewa na mbunge huyo.

“Kilichonifanya niyaseme hayo ni kutokana na kauli ya rafiki yangu kipenzi Sugu kuingilia mchango wangu. Mimi ni ‘human being’ nina ‘character’ zote tatu, hivyo aliponiingilia, zikani ‘drive’ na kusema niliyosema.

“Sugu ni rafiki yangu na nyimbo zake ninazo, namuomba radhi na nitaendelea kusikiliza nyimbo zake,” alisema Nkamia.

Credit:Mtanzania

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate