MKAZI wa Chang’ombe, jijini Dar es Salaam, Tumaini Allen Mbepo, maarufu
kwa jina la mama Tuma (47), amepandishwa kizimbani kwa kosa la kumtukana
Godfrey Chrisant, aliyemkataa kimapenzi.
Mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka hayo jana, mbele ya Hakimu Haji Mbaga wa Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Temeke.
Ilidaiwa mahakamni hapo kuwa mshitakiwa huyo mnamo Februari 20, mwaka huu, kwa makusudi ulimtukana Godfrey bila ya aibu, kwa sababu ya kukataliwa kimapenzi, huku akijua kufanya hivyo ni kosa.
Mshitakiwa alikana kosa hilo na kudai kuwa yeye na Godfrey waliingia mkataba hivyo ni mpangaji wake na si mpenzi wake.
“Hakimu huyu ni mpangaji wangu na ametakiwa alipe kodi hajalipa mpaka sasa, ndio maana nimemtukana matusi, ila si mpenzi wangu,” alidai mshtakiwa huyo.
Kwa upande wa dhamana ilikuwa wazi ambapo mshitakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni wafanyakazi wa Serikali.
Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana hadi kesi yake itakapotajwa tena Aprili 17, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza mashahidi.Mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka hayo jana, mbele ya Hakimu Haji Mbaga wa Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Temeke.
Ilidaiwa mahakamni hapo kuwa mshitakiwa huyo mnamo Februari 20, mwaka huu, kwa makusudi ulimtukana Godfrey bila ya aibu, kwa sababu ya kukataliwa kimapenzi, huku akijua kufanya hivyo ni kosa.
Mshitakiwa alikana kosa hilo na kudai kuwa yeye na Godfrey waliingia mkataba hivyo ni mpangaji wake na si mpenzi wake.
“Hakimu huyu ni mpangaji wangu na ametakiwa alipe kodi hajalipa mpaka sasa, ndio maana nimemtukana matusi, ila si mpenzi wangu,” alidai mshtakiwa huyo.
Kwa upande wa dhamana ilikuwa wazi ambapo mshitakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni wafanyakazi wa Serikali.
“Kuna askari mmoja mse…… amekuja kunishitaki mahakamani, anadhani atashinda, haniwezi, nitamfunga,” alisikika mama huyo akizungumza kwa simu mara baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo.
No comments:
Post a Comment