MWIGIZAJI wa kike Irene Bahati Paul anayefanya vinzuri katika tasnia ya
filamu Bongo amedai kuwa ameachana na kazi ya utangazaji baada ya
kubaini kuwa filamu inamlipa kuliko fani ya utangazaji aliyekuwa
akifanya na kubaini kuwa maslahi kwake ni madogo tofauti na alipojiunga
na uigizaji kwa muda mfupi tu faida kaiona.
Kwangu mimi filamu inanilipa na imekuwa nimeamua kuachana na kazi
nyingine zote ili niwe makini na kazi ya uigizaji ambayo naona maslahi
ya moja kwa moja na ni kazi ambayo ninaipenda sana imenikutanisha na
watu mbalimbali marafiki pia imebadilisha maisha yangu napata
ninachohitaji bila wasi wasi,”anasema Irene.
Irene alianza kutangaza katika televisheni ya C2C na baadae Clouds Tv
na kuachana na kazi hiyo ya utangazaji kuingia katika uigizaji baada ya
kukutana na Ray na kupewa nafasi ya uigizaji, msanii huyo pia
amewashukru Zamaradi Mketema kwa kumshauri kuingia katika uigizaji kwani
aliona kipaji chake.
Msanii huyu ameshiriki filamu na wakongwe katika tasnia ya filamu
Kanumba na Ray, filamu alizoigiza ni I hate my Birthday, Kibajaji, More
than Pain, Kalunde filamu aliyoitengeneza mwenyewe na
imeonekana kufanya vizuri sokoni.
imeonekana kufanya vizuri sokoni.
No comments:
Post a Comment