Omar Borkan Al Gala, mwigizaji na pia mpiga picha wa huko Dubai 
ambaye kwa mujibu wa taarifa, yeye pamoja na wenzake wawili wamefukuzwa 
huko Saudi Arabia kutokana na kuwa na muonekano mzuri kupitiliza (Yaani 
ma-handsome kupita kiasi) ili kuepusha kuwaingiza katika tamaa wanawake 
ambao hushindwa kujizuia kuwashobokea.
Omar
 alitolewa na maafisa wa polisi na kunyimwa kuhudhuria katika tamasha 
ambalo hufanyika kila mwaka nchini humo ambalo huusisha mbio za Ngamia, 
Janadriyah Festival ambalo kwa sehemu kubwa huhudhuriwa na matajiri, na 
baadhi ya vyanzo vya taarifa vinasema Omar alitolewa kutokana na mualiko
 wa msanii wa kike maaruku kutoka Falme za Kiarabu ambaye walihofia 
angeweza kutengeneza mahusiano naye.... na wengine wakisema ni hofu ya 
wakubwa kuibiwa mademu wao. 
 
 
 
 
 
 
 



 
No comments:
Post a Comment