*Atuhumiwa kughushi hati ya Sh mil 500/-
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke, mkoani Dar
es Salaam, Ayoub Chamshama na mwanaye, Saidi Ayoub Chamshama,
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa
tuhuma za kughushi na kujipatia Sh milioni 500. Washtakiwa hao,
walipandishwa kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi, Geni Dudu na
kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Charles Anindo.
Akisoma mashtaka hayo, Anindo alidai washtakiwa wote wanakabiliwa na shtaka la kula njama kutenda kosa tarehe na mahali pasipofahamika mjini Dar es Salaam.
“Shtaka la pili, linamkabili mshtakiwa Ayoub, anadaiwa Oktoba 16, 2007 jijini Dar es Salaam, alighushi hati ya dhamana ya nyumba ya familia, plot namba 12 iliyopo maeneo ya Jangwani, kiwanja namba 28181.
“Mheshimiwa, mshtakiwa alijifanya mmiliki halali wa nyumba hiyo, huku akijua anachokifanya si kweli na kosa kisheria.

“Katika shtaka la tatu, washtakiwa wote wawili wanadaiwa kuwasilisha nyaraka hizo za kughushi katika Benki ya KCB, kwa ajili ya kupata mkopo,” alidai Anindo.
Alidai shtaka la nne kwa washtakiwa wote, wanadaiwa walijipatia Sh milioni 500 kutoka benki ya KCB, baada ya kutoa hati ya kughushi ikionyesha mmiliki wa nyumba hiyo ni Abdi Ali Salehe.
Inadaiwa katika shtaka la tano, Mwenyekiti Ayoub, Oktoba 16, 2007, akiwa na nia ya kudhulumu na kujipatia manufaa alijitambulisha ni Abdi Salehe kwa wakili wa kujitegemea, Silvester Shayo.
Anindo, aliwataka washtakiwa kujibu mashtaka yanayowakabili, lakini wote walikana kutenda makosa hayo, upelelezi wa kesi haujakamilika.
No comments:
Post a Comment