Mwenyekiti
Taifa wa Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA), Hassan Mchanjama,
akizungumza na waandishi wa habari jijini jana kuhusu kupinga
kupandishwa kwa nauli kulikofanywa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti
wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA)
*Wadau watangaza kuishitaki SUMATRA mahakamani
*Wamiliki wa mabasi wasema nchi itakosa usafiri
SAKATA la ongezeko la nauli mpya za daladala na mabasi yaendayo mikoani, sasa ni wazi kuwa limegeuka kuwa kaa la moto. Hali hiyo inajitokeza baada ya Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA), kutangaza kusudio la kuishitaki Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kwa hatua yake hiyo.

Uamuzi huo ulitangazwa na Mshauri wa Idara Kuu ya Huduma ya Maoni ya
chama hicho, Wilson Mashaka wakati akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana.
Mashaka alisema chama chake kinakusudia kuishitaki SUMATRA, kutokana na kupandisha nauli kiholela bila kushirikisha wadau wa usafiri, jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu.

Mashaka alisema sababu na vigezo vilivyotumika kuishawishi SUMATRA kufanya mabadiliko hayo ya nauli, hazina msingi wala mashiko mbele ya jamii.
“Hizi nauli zimepandishwa kwa hila na nia ya kuweka rehani maisha ya wananchi masikini ambao hawana uwezo wa kumiliki usafiri kama watu wengine.
“Suala la usafiri ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi kwenda mahali popote anakotaka, kwa kulipa nauli inayofaa na linganifu katika vyombo vya usafiri,” alisema.
“Madai ya kupata hasara kutoka kwa wamiliki yasiyokuwa na ukweli siku zote yanaaminika kwa SUMATRA tu, kwani taarifa ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha ya wamiliki wa mabasi haijatolewa.
“Maamuzi ya kupandisha nauli hizo hayakuzingatia ukweli kuwa wamiliki wa mabasi wana mfumo mbaya wa kuwagawia pesa wapiga debe na askari traffic barabarani.
“Sasa fedha hizo ambazo hutolewa kiholela, wamiliki wanataka zilipwe na wananchi, huo ndiyo msingi wa wamiliki wa mabasi kutaka abiria wapandishiwe nauli ili kufidia,” alisema.
SUMATRA ifutwe
Alisema umefika wakati kwa chombo hicho kufutwa na kuundwa kingine, kwani SUMATRA imekuwa ikijali zaidi maslahi ya watoa huduma na kusahau kulinda maslahi ya wananchi.
Mashaka alikanusha taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo kwamba, hatua ya kutangaza ongezeko la nauli mpya iliridhiwa na wadau wote wa usafiri.
“Katika kikao hicho kinachodaiwa kufanyika Septemba na Novemba mwaka jana, sisi CHAKUA kama chama cha kutetea maslahi ya abiria hatukushirikishwa.
“Nauli zimepandishwa kwa kigezo kisichokubalika wakidai kuwa wataleta mabasi mapya bila kuwepo uthibitisho wa mchakato huo kimkataba.
“SUMATRA wamepandisha nauli bila ya kuuthibitishia umma na abiria, kuwepo kwa kiwango bora cha uwekezaji na orodha ya wawekezaji makini wenye ushindani na huduma salama kwa abiria.
Alisema sheria ya usafirishaji ya mwaka 2001, inazuia mamlaka yoyote kutangaza ongezeko la nauli za mabasi, reli na meli kwa wakati mmoja bila kuwaelimisha kwanza wananchi kuhusu ulazima wa kufanya hivyo.
Hata hivyo, Mashaka alisema uongozi wa SUMATRA unapaswa kuwajibishwa kutokana na kusababisha usumbufu na kuzua hofu na mkanganyiko kati ya wananchi na Serikali.
Chama hicho kimemwomba Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kupitia upya uamuzi uliotolewa na SUMATRA ili kuwasaidia wananchi wanyonge.
“Pia tunapendekeza sheria ya SUMATRA namba tisa ya mwaka 2013, irekebishwe kwa kufuta kipengele kinachowapa nguvu ya maamuzi SUMATRA. Hawa jamaa si mahakama kuu ni watendaji tu,” alisema.
TABOA yatoa vitisho
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (TABOA), Enea Mrutu, alikishangaa chama hicho kutoa malalamiko.
Hata hivyo, Mrutu alisema tangazo la kuanza kutumika kwa viwango vipya vya nauli Aprili 12, lipo pale pale na kwamba nauli hiyo isipotumika nchi itaparalaizi (huduma ya usafiri itakwama).
“Kwanza ujue Chakua siku zote ni wapinzani wetu katika suala la nauli. Nashangaa wanapinga hatua ya ongezeko la nauli, wakati wao wenyewe walishiriki katika kupitisha uamuzi huu.
“Chakua walishiriki katika mkutano wa kujadili ongezeko la nauli za mabasi ya abiria, wadau wote walishiriki katika mkutano uliofanyika Novemba, mwaka jana na taratibu zote zilifuatwa.
“Kwa hiyo katika suala hilo hakuna jambo lililokiukwa katika mchakato wa ongezeko la nauli. Sisi tunasema hivi sababu zetu za kutaka nauli ipandishwe ni za msingi, nataka uelewe hivyo.
“Kwa hiyo msimamo wetu ikifika Aprili 12, kama ilivyotangazwa nauli mpya ipo pale pale na endapo nauli mpya hazitatumika kama ilivyotangazwa bila shaka nchi ita paralyze (itayumba),” alisema Mrutu.

SUMATRA yatetea msimamo
Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa SUMATRA, David Mziray, alipotafutwa kuzungumzia suala hilo aliwapuuza Chakua na kusema utaratibu umefuatwa katika suala hilo.
Kuhusu mamlaka yake kupelekwa mahakamani alisema hilo ni jambo la kawaida na kwamba sheria inaruhusu mdau yeyote kwenda mahakamani iwapo hajaridhika na uamuzi wa SUMATRA.
“Kama wao wanakwenda mahakamani kutushitaki waende, kwani sheria inaruhusu kama mtu hajaridhika na ongezeko la nauli ni haki yake ya msingi kabisa kwenda mahakamani.
“SUMATRA ni msimamizi anayezingatia maslahi ya pande zote mbili bila kumwonea mtu. Hatutaki kumuumiza mmoja halafu mwingine aachwe.
“Sisi tuko kati kuhakikisha kila upande unanufaika. Kuhusu ule mkutano ni kwamba wadau wote walishiriki wakiwamo Chakua waliwasilisha hata mapendekezo yao,’ alisema.
Mziray alisema, haoni sababu za kuilaumu mamlaka yake kwani wamiliki wa mabasi ya abiria walitaka nauli ipandishwe kwa asilimia 149, lakini SUMATRA ilipinga na kuruhusu ongezeko la asilimia 24 tu.
“Katika kuongeza nauli hizo tuliangalia mambo mengi na kuna kanuni kabisa za ukokotoaji wa nauli hizo, kuna mambo mengi tunaangalia kama inflation (mfumuko wa bei), gharama za uendeshaji, bei ya mafuta na vitu kama hivyo.
“Kwa hiyo tunazingatia pia mtoa huduma ataweza kuendelea kutoa huduma hizo katika mazingira kama hayo. Kama mtakumbuka hata mwaka 2008, nauli zilipungua, huu ni mchakato unaofuata utaratibu wa kawaida.”Wananchi wapinga
Baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam, wameungana na wabunge kupinga uamuzi wa mamlaka hiyo kuongeza nauli.
Miongoni mwa wabunge waliojitokeza kupinga ongezeko hilo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM) na Mbunge wa Tunduru Kusini, Mtutura Abdallah Mtutura (CCM).
Akitoa maoni yake jana, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kambangwa, Amosi Mpinga, alisema SUMATRA imekurupuka kutangaza ongezeko la nauli.
Alisema katika hali ya kawaida, ni vema ongezeko la nauli liende sambamba na ongezeko la mishahara na upatikanaji wa ajira ili wananchi waweze kumudu gharama hizo za maisha.
“Kama wataongeza nauli kila mahali wajue kuwa kuna wananchi wengine watashindwa hata kufika sehemu zao za kazi, hivyo taifa halitasonga mbele kama wafanyakazi wake watakaa bila kazi.
“Hivyo ni vema basi wafanyakazi nao waongezewe mishahara na wale ambao hawana ajira watafutiwe namna ya kuwezeshwa, ili wamudu viwango hivyo,” alisema Mpinga.
Naye, Pendo Paulo mkazi wa Kurasini anayeshughulika na kazi ya ulinzi, alisema SUMATRA imeshindwa kuangalia suala hilo kwa kuzingatia hali halisi ya maisha ya Mtanzania wa kawaida.
“Haya si maisha bora, kama nilikuwa natumia kiasi cha Sh 5000 kwa siku, ina maana itaongezeka kwani nina familia, sasa nauli itakapoongezeka halafu mshahara ni ule ule nitapata wapi fedha hizo?
“Kuna rasilimali nyingi katika nchi hii, ni kwa nini wasiamue kuchukua kiasi cha fedha wakaongezea wanatupandishia sisi gharama za nauli, hali hii itazidi kutuumiza kwa sisi wenye uwezo mdogo,” alisema.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Ahmed Kilima juzi alitangaza mabadiliko ya viwango vya nauli mpya za daladala na mabasi yaendayo mikoani, kulingana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji.
Habari hii imeandikwa na Chresencia Augustine, Winfrida Rwegasira na Maneno Salanyika.

No comments:
Post a Comment