Na Musa Mateja wa Global Publishers.
NI kivumbi! Kuna madai kwamba, staa wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani mbalimbali, Ijumaa limeinyaka.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.
Mbali
na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema
aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye
inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa
msanii huyo.
“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao
wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika
mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa
huyo,” kilisema chanzo.
Haikujulikana mara moja ni kitu gani
kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda
kwa Wema na kutenda kosa hilo.
Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.
Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.
No comments:
Post a Comment