Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu)
amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete asiitumie ziara yake ya Mkoa wa
Mbeya kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi(CCM) bali afanye kazi za
kiserikali.
Rais Kikwete anatazamiwa kuwasili mkoani Mbeya, Jumapili ijayo kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana Mjini Mbeya,Sugu alisema kuwa kitendo hicho kitasaidia kuimarisha umoja miongoni mwa wananchi wa Mbeya.
“Wakazi wa Mbeya muwe tayari kumpokea Rais Kikwete endapo ataifanya ziara yake kuwa ya kiserikali na yeye akiwa ni rais wa nchi na siyo kuifanya ziara hiyo kuwa ya kisiasa kwa vile tu yeye ni mwenyekiti wa CCM,”alisema Sugu.
Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Ruanda-Nzovwe, ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Wilbroad Slaa, Mbunge wa Iringa, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa mjini), Ezekiel Wenje(Mwanza mjini) na Highness Kiwia wa Jimbo la Ilemela. Sugu pia alitoa miezi mitatu kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha Soko Jipya la Mwanjelwa linakamilika ifikapo Julai mwaka huu.
Alitishia iwapo kufikia muda huo halijakamilika yeye na wananchi wenzake watavamia soko hilo na kufanya kazi za ujenzi wenyewe.
Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Peter Msigwa alisema kuwa wamejipanga kufanya maamuzi magumu kama Spika wa Bunge, Anne Makinda
ataendelea kuwapendelea wabunge wa CCM.
Dk Willbroad Slaa alisema sababu ya wabunge wa Chadema kufukuzwa bungeni ni
kutokana na kutekeleza majukumu waliyotumwa na wananchi.
Aliwataka Wananchi kuendelea kuwaunga mkono na watambue kuwa CCM na Serikali yake inafanya kazi ya kutetea ubovu wa Serikali na kuwafanya Watanzania kuwa katika hali ya
umasikini huku walionacho wakizidi kuneemeka.
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliosimamishwa bungeni wiki iliyopita wameamua kwenda kuwashitaki Spika Anna Makinda na Naibu wake Job Ndugaikwa wananchi kwa njia ya kuitisha mikutano ya mihadhara.
No comments:
Post a Comment