Rais wa Sudan Omar al Bashir, ameagiza kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa vikao vipya
vya bunge, Rais Bashir alitoa wito wa kufanyika mashauriano na vyama
vingine vya kisiasa.
Wiki jana makamu wa rais Ali Osman Taha
aliwaalika waasi kutoka majimbo ya Kordofan Kusini na Blue
Nile,kushauriana kuhusu katiba mpya.
Hata hivyo walikataa mwaliko huo.
Waandishi wa habari wanasema kuwa hali ya
wasiwasi imeanza kupungua kati ya Sudan na Sudan Kusini tangu nchi hizo
mbili zikubaliane kurejelea shughuli ya kuchimba na kusafirisha mafuta.
No comments:
Post a Comment