MWENYEKITI wa Kamati ya Uendelezaji wa
jengo dogo la Yanga SC, liliopo Mtaa wa Mafia, Kariakoo, Dar es Salaam,
Ridhiwani Jakaya Kikwete ameteua Wajumbe kadhaa wa kumsaidia kazi hiyo,
wakiwemo wanasheria wawili na wataalamu wa Taasisi za Fedha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya
klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Ridhiwani alisema katika
uteuzi wa Kamati hiyo, amezingatia utaalamu, uzoefu na mahusiano mazuri
na watu.
Ridhiwani mesema kwamba kutakuwa na
Kamati mbili za kushughulikia mchakato huo, moja ikiwa ya wataalamu na
nyingine ya watendaji.
Aliwataja Wajumbe wa Kamati
ya Wataalamu kuwa ni Makamu wake, Issa Hajji Ussi na Wajumbe Isaac
Chanji, Mbaraka Igangula, Jaji John Mkwawa, mtumishi ya Beki ya
Uwekezaji Tanzania (T.I.B.), Alan Magoma, Mwanasheria mkongwe, Mavale
Msemo na mtumishi mwingine wa Benki, Charles Palapala.
“Utaona
kuna watu wengi wa taasisi za fedha, kwa sababu hili zoezi linahitaji
fedha, tutaangalia kama tutaingia ubia na mtu, au sisi kama klabu
tukawekeza kwenye mradi huo moja kwa moja,”alisema.
Kwa
upande wa watendaji, Kikwete alisema kwamba Kamati yao itaongozwa na
Katibu wa Yanga SC, Lawrence Mwalusako, Beda Tindwa na Mahmoud Milandu.
“Kamati
yetu sisi itakuwa ya kukaa na kutengeneza mipango na baadaye kama
kutakuwa na barua ya kupeleka wapi, au mtu wa kufuatwa, basi ile kamati
nyingine ndogo, itafanya kazi hiyo,”alisema.
Credit: Mahmoud Zubery (bongostaz)
No comments:
Post a Comment