Taarifa kutoka Mbeya zinaripoti kutokea vurugu huko Tunduma
zilizosababisha mtu mmoja kujeruhiwa, kutokana na mchanganyiko wa
masuala ya kiimani katika uchinjaji wanyama baina ya Wakristo na Waislam
na kwa upande mwingine “wapiga debe” waliochochea kukuza mambo kwa
sababu wanazozijua wenyewe.
Mwandishi wa habari aliyeko eneo hilo, Moses Ng'wat ameieleza blog ya blogu ya FrancisGodwin kuwa vurugu hizo zilianza majira ya saa 4 asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa viongozi wa dini ya Kikristo, Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa Wilaya ya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa sikukuu ya Psaka.
Alisema kuwa kabla ya siku ya Ijumaa Kuu, viongozi hao wa dini ya Kikristo walikutana na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Abood Saibea ambaye aliwataka kuwasilisha barua rasmi .
Uchinjaji ulifanyika siku ya Pasaka na hapakuwa na mvutano wowote baada ya Wakristo kuchinja katika bucha zao na Waislamu kuchinja katika bucha zao na kila mmoja kufanya biashara kwa kupata wateja wake kama kawaida.
Lakini katika hali ya kushangaza, leo kuliibuka kundi la vijana wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbalimbali, na kuanzisha vurugu kiasi cha kuwalazimu Polisi wa FFU kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali.
Kutokana
na vurugu hizo mpaka wa Tunduma ambao unaingia nchi za kusini wa
Tanzania ulifungwa. Magari yaliyokuwa yakitoka Sumbawanga
pia yalizuiwa kuendelea na safari kwa muda hadi hali ilipotengamaa
majira ya saa 8 mchana pale kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani
Athuman alipofika katika eneo hilo.Mwandishi wa habari aliyeko eneo hilo, Moses Ng'wat ameieleza blog ya blogu ya FrancisGodwin kuwa vurugu hizo zilianza majira ya saa 4 asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa viongozi wa dini ya Kikristo, Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa Wilaya ya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa sikukuu ya Psaka.
Alisema kuwa kabla ya siku ya Ijumaa Kuu, viongozi hao wa dini ya Kikristo walikutana na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Abood Saibea ambaye aliwataka kuwasilisha barua rasmi .
Uchinjaji ulifanyika siku ya Pasaka na hapakuwa na mvutano wowote baada ya Wakristo kuchinja katika bucha zao na Waislamu kuchinja katika bucha zao na kila mmoja kufanya biashara kwa kupata wateja wake kama kawaida.
Lakini katika hali ya kushangaza, leo kuliibuka kundi la vijana wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbalimbali, na kuanzisha vurugu kiasi cha kuwalazimu Polisi wa FFU kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali.
Kwa ujumla inaripotiwa kuwa hakuna madhara makubwa yaliyotokana na vurugu hizo.
Hii ni taarifa za awali tu kadiri zinavyoripotiwa na walioko kwenye eneo. Ikipatikana taarifa rasmi, itawekwa hapa kama “update/taarifa mpya”. Tafadhali fuatiliakwenye vyombo vya habari rasmi kwa taarifa sahihi kadiri zitakavyopatikana kutoka Jeshi la Polisi na vyombo vingine vyenye dhamana.
No comments:
Post a Comment