Jana ilikuwa ni siku ya uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katiba ngazi ya
Mtaa ambapo Dar ilifanyika jana na huo ni sehemu moja wapo ya Wakaazi wa
Mtaa waliojitokeza kwenye uchaguzi huu ambao niliushuhudia na kushiriki
kikamilifu.


Mmojawapo
wa Wagombea, Abdulhaman Kasim Ngamba akinadi sera zake ambapo mwisho wa
siku aliibuka mshindi wa kwanza wa jumla kwa kundi la vijana na kwa
washiriki wote.

Mgombea
mwingine Marry Chilala akinadi sera zake kwa Wananchi ambapo naye pia
aliibuka mshindi wa pili wa ujumla na mshindi wa kwanza kwa upande wa
kundi la Wanawake.

Mgombea
mwingine Emmanuel John akinadi sera zake kwa umma ambapo naye pia
aliibuka mshindi wa pili kwa upande wa kundi la vijana na mshindi wa
tatu kwa makundi yote. Kijana yupo safi.

Mgombea Emmanuel John akipiga kura.

Ulifika wakati wa zoezi zima la kuhesabu kura ukawadia.

Hapa
Emmanuel John akitangazwa Mshindi wa Mjumbe wa Baraza la Katiba Mamlaka
ya Serikali za Mitaa kutokana na uamuzi wa kura za Wananchi.

Kuna jamaa alipanda jukwaani kuja kumpongeza Emmanuel John kwa ushindi alioupata.

Mtu wa watu, Emmanuel John akipongezwa na Wananchi kwa ushindi wa kishindo aliouvuna.

Kadri muda ulivyozidi kusonga kila mdau alikuwa na hamu ya kupiga picha na Emmanuel John.


Wakazi waliojitoza kwenye zoezi zima la uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katiba Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Via MO Blog
No comments:
Post a Comment