MWIGIZAJI na muongozaji wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameamua
kuvunja ukimya na kudai kwamba kupungua kwake mwili sio kwamba anaumwa
bali ni katika kubadilisha muonekano wake.
Akifunguka katika kipindi cha ‘Action Cut’ kinachorushwa na Chanel
Ten, Ray alisema kumekuwepo na maneno mengi yanasemwa na watu na mengine
kumfikia kuwa kuna kitu kinamuuma, hivyo ni bora aombe msaada mapema
ili aweze kusaidiwa.
“Jamani nataka kuwahakikishia mashabiki wangu kuwa sina panaponiuma
bali nimeamua kuutengeneza tu mwili wangu kama wafanyavyo mastaa wa nje
na kutokana na hali hii, sasa hivi naweza kucheza nafasi mbalimbali,
ikiwemo kupigana, mwanafunzi na wategemee kuniona katika aina nyingine
ya uigizaji na siyo ile waliyonizoea,” alibainisha Ray.
No comments:
Post a Comment