Kutokana na vurugu hizo, Chuo cha Uhasibu cha Arusha, kimefungwa kwa muda usiojulikana kwa usalama huku wanafunzi wakitakiwa kuondoka chuoni hapo hadi watakapotangaziwa tena.
Gari ya Mh.Godbless Lema ikiochukuliwa na polisi kutoka eneo la tukio
Licha ya kuelezwa kwamba aliuawa kwa kisu,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alisema taarifa nyingine,
zinaeleza kuwa aliuawa akitokea katika Ukumbi wa Disko wa Bugaloo jirani
na chuo hicho.
Baada ya taarifa za kifo hicho, wanafunzi wa chuo hicho walikusanyika jana asubuhi na kuanza maandamano hadi Kituo Kikuu cha Polisi wakilalamikia ulinzi duni.
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alifika na kuwatuliza wanafunzi hao na kuzungumza nao, kwa zaidi ya saa tatu wakati wakimsubiri Mkuu wa Mkoa.
Hata hivyo, baada ya kufika chuoni hapo, mkuu huyo wa mkoa alishindwa kuzungumza kutokana na kutokuwa na kipaza sauti na kusababisha wanachuo kumzomea kabla ya uongozi wa chuo kubadili eneo la mkutano. Hata hivyo, zomeazomea iliendelea na mkutano kuvunjika na FFU kufika na kurusha mabomu ya machozi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na uongozi wa chuo hicho, mkuu huyo wa mkoa alisema polisi wanafanya uchunguzi wa suala hilo.
“Baada ya kuletewa taarifa za tukio hili na Mbunge Lema, niliondoka na kwenda kuwasikiliza wanachuo lakini tayari nilijua mazingira yalikuwa yamebadilishwa na pale nikagundua Lema ndiyo amekuwa msemaji mkuu badala ya uongozi wa chuo au Serikali ya wanachuo. Ndiyo maana mkaona na zomeazomea ile,” alisema Mulongo.
Alimtuhumu mbunge huyo uchochezi na ameamuru kukamatwa kwake na wanafunzi waliohusika na vurugu zile.
Lema alieleza kusikitishwa na agizo la kutakiwa kukamatwa akisema alizuia maandamano kufika mjini... “Nyie waandishi wa habari mlikuwepo nimezungumza zaidi ya saa mbili na wale wanafunzi kuwasihi watulie wasiandamane na mimi ndiye nilimpigia simu Mkuu wa Mkoa aje kuwasikiliza wanafunzi iweje niwachochee kufanya fujo? Ninawasubiri waje wanikamate.”
Polisi wakichukua gari ya mbunge wa jimbo la Arusha
No comments:
Post a Comment