Hazina hiyo ambayo iliundwa baada ya msichana
huyo kupigwa risasi kichwani na kundi la Taliban mwaka uliopita
itafadhili masomo ya wasichana 40 nchini Pakistan.
Akihutubia
kupitia njia ya Video kutoka London Malala alisema kuwa kuvumbuliwa kwa
hazina hiyo ndio siku yake ya furaha zaidi duniani.

Angelina Jolie msanii wa filamu
Bii Angelina Jolie amesema kuwa Malala mwenye umri wa miaka 15 ndiye atakayesimamia hazina hiyo na matumizi yake.
Hii itagharimu zaidi ya dola elfu arobaini na
tano. Hazina hiyo ilianzishwa na Malala, kwa ushirikiano na wanaharakati
wa elimu ya wasichana, mashirika yasiyo ya kiserikali na Umoja wa
mataifa.
Kufikia sasa imekusanya dola nusu milioni, huku mchango mkubwa ukitoka kwa Angelina Jolie.
Hata hivyo bado ni wazi kuwa wasiwasi umetanda mjini Swat.
Hazina hiyo haijatangaza hadharani ni shule zipi
zitakazofaidi na fedha hizo kwa hofu kuwa huenda zikashambuliwa na
wanamgambo wa Taleban.

No comments:
Post a Comment