EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, April 6, 2013

Chadema wajipanga kumbana Pinda ripoti za uchunguzi

Dar es Salaam, 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimejipanga kutumia Bunge la Bajeti, kumpana Waziri Mkuu Mizengo Pinda, azitoe ripoti za kamati kadhaa zilizowahi kuundwa kufuatilia masuala elimu nchini.
 
Pia uongozi wa Chadema umepania kutumia nafasi hiyo kuwasilisha bungeni, nyaraka zinaonyesha jinsi Kampuni ya Jitegemee,
inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ilivyopewa mamilioni ya fedha kwa namna ya ufisadi.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya chama hicho.
Kamati hiyo imekuwa na kikao kilichotarajiwa kumalizika juzi, lakini kimeongezwa siku zaidi.


“Kamati Kuu ya Chadema imelazimika kuongeza siku za kukutana hadi leo (jana), tupo hapa kutokana na wingi wa agenda zilizopo, ambazo ni pamoja na hili suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne na hatua ambazo Serikali imezichukua hadi sasa,” alisema Mnyika.
Alifafanua kuwa Kamati Kuu ya Chadema, haijakubaliana na hatua ya Serikali ya kuunda tume nyingine ya kuchunguza chanzo cha matokeo
hayo na kushindwa kumwajibisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.

Alisema chama hicho kinatambua kwamba kumeshawahi kuundwa kamati nyingi ikiwamo ile ya mwaka 2010 na nyingine mwaka 2011 ambazo hadi leo, Serikali haijawahi kutoa ripoti ya matokeo ya uchunguzi kwa wananchi.
“Kamati imewataka wabunge kutumia nafasi ya Bunge la Bajeti, kuwasilisha hoja za kumtaka Waziri Mkuu kuzitoa ripoti hizo, kupitia Kambi ya Upinzania Bungeni inayoongozwa na Chadema, tutahakikisha kuwa tunafanikisha lengo letu kwa kuzingatia kanuni za Bunge,” alisema.

Viongozi wa Chadema kwa nyakati tofauti walitangaza kufanyika kwa maandamano yaliyolenga kumshinikisha Dk Kawambwa na Naibu wake Philipp Mulugo, kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya mitihani ya kidato cha nne mwaka jana.

Hata hivyo, polisi walizuia kufanyika kwa maandamano hayo kwa maelezo kuwa tayari Serikali imeunda tume inayoongozwa na Profesa Sifuni Mchome, kushughulikia suala hilo.
Mnyika alisema baada ya kuwasilisha hoja hizo bungeni na hatua zinazostahili hazitachukuliwa, watalazimika kuandaa maandamano ili kushinikiza uwajibikaji wa viongozi hao.

Aidha, Mnyika alitumia fursa hiyo kuipongeza CCM kwa kukiri kuwa ndiyo wamiliki wa Kampuni ya Jitegemee, ambayo alidai kwamba inatumika kwa ufisadi.
Chama hicho kimedai kuwa zipo nyaraka za Serikali zinazothibitisha madai namna Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilivyowekeana mikataba ya maegesho na kampuni hiyo.
Chadema pia imemtuhumu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kuwa ametoa zabuni ya ujenzi wa bandari ya nchi kavu kwa kampuni hiyo ya Jitegemee kinyume cha sheria za ununuzi.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate