Dodoma/Mtwara.
Wakati mjadala mkali ukitarajiwa kuibuka bungeni leo wakati Serikali itakapokuwa ikiwasilisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, joto limezidi kupanda mkoani Mtwara ikielezwa kuwa wananchi wamehamasishana kwa mara nyingine kuacha shughuli zote ili kusikiliza kama hotuba hiyo italinda masilahi yao.

Profesa Sospeter Muhongo.
Hotuba hiyo ambayo itasomwa leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni na Waziri wa wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo, inatarajiwa kuibua mengi yakiwamo yanayohusu suala la gesi ya Mtwara.
Mjini Mtwara vipeperushi vinavyopingana vilisambazwa kuhamasishana ‘kuacha shughuli zao zote na kubaki nyumbani ili kufuatilia matangazo ya televisheni wakati Profesa Muhongo atakapotangaza bajeti hiyo, huku vingine vikipinga.
Ahadi za matumaini
Licha ya kampeni hizo za watu wa Mtwara, Serikali
nayo imeweka matangazo katika vyombo vya habari likiwemo gazeti hili
ikieleza namna mikoa ya Mtwara na Lindi itakavyonufaika na utafutaji na
uendelezaji wa Gesi Asilia.
Tangazo lililotolewa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania limeainisha faida za gesi hiyo kwa Mkoa wa Mtwara ukiwamo umeme utakaotokana na gesi asilia. Pia imeelezwa jinsi mafunzo kwa vijana juu ya matatizo ya gesi asilia yaliyodhaminiwa na Wizara ya Nishati na
Madini na kampuni mbalimbali kuanzia mwaka 2010.
Vilevile imeelezwa jinsi uboreshaji wa huduma za
jamii kama ujenzi wa shule, hospitali na ujenzi wa viwanda kama kile cha
saruji cha Dangote na mitambo ya kusafishia gesi utakavyowanufaisha
wakazi wa mkoa huo.
Gesi hiyo ambayo pia inachimbwa katika Kisiwa cha Songosongo inatajwa kwamba itawanufaisha wakazi wa Mkoa wa Lindi kwa kupata umeme, kunufaika na kodi ya wawekezaji wa gesi na udhamini wa mafunzo kutoka kampuni mbalimbali na wizara.
Wiki iliyopita Profesa Muhongo alijigamba kuwa
bajeti ya wizara yake atakayosoma leo itakuwa ya karne ya 22
itakayomaliza tatizo la umeme nchini kwa kuwa imetoa vipaumbele kwa
sekta binafsi kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Mojawapo ya kipeperushi kilisisitiza huduma zote zisitishwe kuanzia bajaji, bodaboda, masoko na magari yote yaendayo mikoani na wilayani yasiingie wala kutoka.
“Sasa Jumatano tena tusifanye biashara. Tuache ujinga Wanakusini wenzetu wengine hawana kazi wala gesi. Kampeni zitafanya tuwe maskini zaidi. Tarehe 22.05.2013 hatufungui duka wala hoteli, hata soko,” kilisomeka kimoja kati ya vipeperushi hivyo.
Dalili za kuibuka mjadala mkali katika bajeti ya leo zilianza
kujitokeza mwishoni mwa wiki wakati wa semina ya wabunge kuhusu masuala
ya gesi ambapo wizara hiyo ilibanwa juu ya mambo ya mikataba.
Hata hivyo, semina hiyo ilitafsiriwa kuwa ililenga
kuwapoza wabunge na kupunguza hasira zao huku wizara ikijipanga namna
ya kuwashawishi waikubali bajeti baada ya kuona mwelekeo wao.
Wasiwasi Mtwara
Hali ya wasiwasi imeanza tena kutanda mkoani hapa
hasa kutokana na vipeperushi vinavyokinzana na ujumbe tofauti kwa njia
ya simu unaosambazwa.
Hali hiyo imejirudia tena huku ikionekana dhahiri
kuwa na kauli kutoka makundi tofauti zinapishana katika vipeperushi
hivyo huku wengine wakitaka mwendelezo wa kusitisha huduma ufanyike na
wengine wakipinga.
Mojawapo ya kipeperushi kilisisitiza huduma zote zisitishwe kuanzia bajaji, bodaboda, masoko na magari yote yaendayo mikoani na wilayani yasiingie wala kutoka.
Huku vipeperushi vingine vikipinga: “Tunafahamu
gesi ni mali yetu wote Wanakusini na tunafahamu kunyanyasika kwetu na
Serikali ya nchi yetu na Mei 17 tuliunga mkono kufunga maduka na
biashara zote, lakini hatukunufaika na chochote.
“Sasa Jumatano tena tusifanye biashara. Tuache ujinga Wanakusini wenzetu wengine hawana kazi wala gesi. Kampeni zitafanya tuwe maskini zaidi. Tarehe 22.05.2013 hatufungui duka wala hoteli, hata soko,” kilisomeka kimoja kati ya vipeperushi hivyo.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Linus Sinzumwa
aliwataka wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku bila kujali
vitisho hivyo kwa kile alichokidai kuwa ulinzi umeimarishwa.
ya za Tandahimba, Masasi, Newala na Nanyumbu waliendelea na shughuli za uzalishaji bila bughudha zozote.Imeandikwa na Haika Kimaro, Mary Sanyiwa na Habel Chidawali.

No comments:
Post a Comment