Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahidi kutumia ushawishi wa
kiuchumi wa nchi yake, kuuzuia Umoja wa Ulaya usiziwekee vikwazo vya
ushuru baadhi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China, ili kuepusha vita vya
kibiashara.
Kansela Merkel aliyasema hayo katika mkutano wa waandishi wa habari
mjini Berlin jana jioni, akiwa na waziri mkuu wa China, Li Keqiang,
ambaye yuko ziarani nchini Ujerumani.
''Ujerumani itapigia debe mazungumzo ya kina kati ya Umoja wa Ulaya na China, kutafuta suluhisho katika tofauti zao za kibiashara haraka iwezekanavyo.'' ameyasema Kansela Merkel, ambaye nchi yake ndiyo yenye uchumi imara zaidi barani Ulaya, akiwa na mgeni wake, waziri mkuu wa China, Li Keqiang, mjini Berlin.
Ujumbe usio sahihi
Umoja huo umependekeza paneli kutoka China ziwekewe ushuru wa kiwango cha asilimia 47, na unaendelea kutafakari hatua za kuchukua dhidi ya vifaa vya mawasiliano. Waziri Mkuu Li amepinga vikali hatua hizo, na kusema zinatuma ujumbe usio sahihi.
''Maoni yetu kuhusu kuweka vizingiti vya masoko, ni kuwa hatua hiyo inawaharibia wengine bila kuleta manufaa kwa aliyeichukua. Hususan ukizingatia mazingira ya utandawazi, hatua hizo hazitaleta mafanikio yoyote. Hatua hizo ni za kutiliwa mashaka, hasa wakati huu ambapo mgogoro wa kifedha haujapatiwa ufumbuzi, na bado uchumi wa dunia haujaweza kusimama kwa miguu miwili.'' Amesema Li.
Umoja wa Ulaya ni mshirika wa pili kwa ukubwa kwa China kibiashara baada ya Marekani, na thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili ilifikia euro bilioni 430 mwaka 2012. Biashara ya paneli za nishati ya jua ilikuwa asilimia 7 ya bidhaa kutoka China zilizouzwa barani Ulaya. Umoja wa Ulaya unatarajiwa kufanya maamuzi juu ya uchunguzi kuhusu bidhaa zinazorundikwa kwenye soko lake, baada ya mashauriano na wadau wote ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Ujerumani yaahidi kukinga kifua
Ujerumani ni nchi pekee ya Umoja wa Ulaya aliyoitembele Li Keqiang, katika ziara hii ambayo ni ya kwanza nje ya nchi tangu alipochaguliwa kuchukuwa wadhifa wa waziri mkuu wa China mwezi Machi mwaka huu, na hilo limechukuliwa kama hatua ya makusudi kutaka kutumia nguvu za Ujerumani kiuchumi kushawishi maamuzi ya Umoja wa Ulaya.
Makampuni makubwa ya kijerumani yanapinga vikwazo kwa China, yakiohofia kuwa kushamiri kwa mzozo wa kibiashara kwaweza kuudhuru uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Wakati wa ziara yake waziri mkuu wa China na kansela Merkel wamefanya mazungumzo na wanafunzi kutoka pande mbili, na kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kiuchumi. Leo hii, waziri mkuu Li Keqiang atakutana na viongozi wa makampuni mbali mbali, na pia atafanya mazungumzo na mpinzani wa Angela Merkel katika uchaguzi wa mwezi Septemba, Peer Steinbrueck.
''Ujerumani itapigia debe mazungumzo ya kina kati ya Umoja wa Ulaya na China, kutafuta suluhisho katika tofauti zao za kibiashara haraka iwezekanavyo.'' ameyasema Kansela Merkel, ambaye nchi yake ndiyo yenye uchumi imara zaidi barani Ulaya, akiwa na mgeni wake, waziri mkuu wa China, Li Keqiang, mjini Berlin.
Halmashauri ya Umoja wa Ulaya wenye nchi 27 wanachama
inaishutumu China kupunguza bei za bidhaa zake kama vile paneli za
nishati ya jua na vifaa vya mawasiliano, kwa makusudi ya kulifurika soko
la Ulaya na kukwamisha ushindani, hali ambayo inayaumiza makampuni ya
Ulaya.
Ujumbe usio sahihi
Umoja huo umependekeza paneli kutoka China ziwekewe ushuru wa kiwango cha asilimia 47, na unaendelea kutafakari hatua za kuchukua dhidi ya vifaa vya mawasiliano. Waziri Mkuu Li amepinga vikali hatua hizo, na kusema zinatuma ujumbe usio sahihi.
''Maoni yetu kuhusu kuweka vizingiti vya masoko, ni kuwa hatua hiyo inawaharibia wengine bila kuleta manufaa kwa aliyeichukua. Hususan ukizingatia mazingira ya utandawazi, hatua hizo hazitaleta mafanikio yoyote. Hatua hizo ni za kutiliwa mashaka, hasa wakati huu ambapo mgogoro wa kifedha haujapatiwa ufumbuzi, na bado uchumi wa dunia haujaweza kusimama kwa miguu miwili.'' Amesema Li.
Umoja wa Ulaya ni mshirika wa pili kwa ukubwa kwa China kibiashara baada ya Marekani, na thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili ilifikia euro bilioni 430 mwaka 2012. Biashara ya paneli za nishati ya jua ilikuwa asilimia 7 ya bidhaa kutoka China zilizouzwa barani Ulaya. Umoja wa Ulaya unatarajiwa kufanya maamuzi juu ya uchunguzi kuhusu bidhaa zinazorundikwa kwenye soko lake, baada ya mashauriano na wadau wote ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Ujerumani yaahidi kukinga kifua
Merkel na Li wakikagua gwaride la heshima
Kansela Merkel amesema pande mbili zinapaswa kuiepusha hali
hiyo. ''Ujerumani itafanya juhudi kuhakikisha tatizo hili linapatiwa
ufumbuzi haraka kama inavyowezekana, kwa sababu hatuamini kwamba vikwazo
vya ushuru vitaleta tija kubwa. Kwa sababu hiyo hatuna budi kufanya
kazi kubwa mnamo miezi sita ijayo, na Ujerumani itahakikisha kwamba
mazungumzo yanapiga hatua.''Ujerumani ni nchi pekee ya Umoja wa Ulaya aliyoitembele Li Keqiang, katika ziara hii ambayo ni ya kwanza nje ya nchi tangu alipochaguliwa kuchukuwa wadhifa wa waziri mkuu wa China mwezi Machi mwaka huu, na hilo limechukuliwa kama hatua ya makusudi kutaka kutumia nguvu za Ujerumani kiuchumi kushawishi maamuzi ya Umoja wa Ulaya.
Makampuni makubwa ya kijerumani yanapinga vikwazo kwa China, yakiohofia kuwa kushamiri kwa mzozo wa kibiashara kwaweza kuudhuru uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Wakati wa ziara yake waziri mkuu wa China na kansela Merkel wamefanya mazungumzo na wanafunzi kutoka pande mbili, na kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kiuchumi. Leo hii, waziri mkuu Li Keqiang atakutana na viongozi wa makampuni mbali mbali, na pia atafanya mazungumzo na mpinzani wa Angela Merkel katika uchaguzi wa mwezi Septemba, Peer Steinbrueck.
No comments:
Post a Comment