Watu wasiopungua 25 wameuawa baada ya wanamgambo wa Muungano wa Seleka
wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kushambulia vijiji kadhaa katika mji wa
Bossangoa ulioko magharibi mwa nchi hiyo.
Taarifa zilizotolewa na
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu zinasema kuwa, miongoni mwa
waliouawa ni wanawake na watoto wadogo.
Wanamgambo wa Seleka ambao hivi
sasa wanashikilia uongozi wa nchi hiyo, wanatuhumiwa kutenda vitendo
kadhaa za jinai ikiwa ni pamoja na uporaji wa mali, mauaji, ubakaji na
unyanyasaji wa raia.
Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu yanasema
kuwa, mara baada ya wanamgambo wa Seleka kumuondoa madarakani Rais
Francois Bozize tarehe 24 Machi mwaka huu, hali ya amani na utulivu
imetoweka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
No comments:
Post a Comment