Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa kocha
wa timu hiyo Jose Mourinho ataondoka kwenye kibarua cha kuifundisha timu
hiyo mwishoni mwa msimu.

Jose Mourinho.
Aidha Madrid, imeongeza kuwa haijaanza mazungumzo na kocha yeyote kwaajili ya kuchukua nafasi ya Mourinho lakini vyanzo mbalimbali vya habari za michezo zinamtaja kocha wa PSG ya Ufaransa, Carlo Ancelloti kuchukua jukumu la kuifundisha Madrid msimu ujao.
Duru za kimichezo zinasema, Jose Mourinho huenda akarejea nchini Uingereza kuifundisha klabu yake ya zamani ya Chelsea baada ya kuwepo makubaliano baina yake na uongozi wa klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment