Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza rasmi matokeo ya Kidato
cha Nne 2012. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne
mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la
Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya
ufaulu.
Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la
kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo
yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57.
Hii inamaanisha
kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri
katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu
katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri
kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya
349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756
waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa
daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4.
Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5
walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo
yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni
asilimia 43.
Ili kupata matokeo hayo kwa urahisi na haraka zaidi tafadhali bofya link inayo onekana hapo chini.
No comments:
Post a Comment