WATU sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha
wamevamia kijiji cha Mwamkulu, kilichoko wilaya ya Mpanda na kupora
vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni tisa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa 2:00 usiku.
Alivitaja vitu vilivyoporwa kwenye tukio hilo kuwa ni pikipiki tatu
zenye namba T964 BUZ aina ya SUNLG, T792 BWT aina ya Kiboko na T 452 BNZ
aina ya Shanray zikiwa na thamani ya sh milioni 5.6.
Vitu vingine vilivyoporwa ni simu 16 za mikononi zenye thamani ya sh
720,000 , pesa taslimu sh milioni mbili za wafanyabiashara, katoni
mbili za sigara zenye thamani ya sh 420,000 na vocha za simu zenye
thamani ya sh 820,000.
Alisema polisi baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walifika na
kufanya msako mkali na kufanikiwa kukamata pikipiki tatu ambazo
zilitelekezwa na majambazi hao baada ya kugundua wanafuatwa na polisi,
simu moja ya Nokia yenye thamani ya sh 45,000 mali ya Shadrack Abel.
Alisema katika tukio hio maganda matano ya risasi aina ya SMG/SAR
yaliokotwa, kwani majambazi hayo yalipiga risasi sita hewani kwa lengo
la kuwatisha wanakijiji hao.
No comments:
Post a Comment