Kibanda, ambaye ni Mwenyekiti wa TEF, alitekwa na watu
wasiojulikana Machi 5, 2013 mwaka huu na kukumbana na mateso karibu na
maeneo ya nyumbani kwake, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Kutokana na hali hiyo, TEF iliamua kuunda timu ya
watu watano kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo na viashiria vya kutishia
usalama wa wanahabari nchini.
Taarifa hiyo, ambayo pia ilisomwa na Mwenyekiti wa
Kamati iliyofanya uchunguzi huo, Deodatus Balile kwenye mkutano wa
wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika mjini Tanga,
imebainisha viashiria mbalimbali vilivyofanya Kibanda kukutana na zahama
hiyo.
Pia imevitaka vyombo vya dola kufanyia kazi ripoti hiyo, ili kufuatilia viashiria vilivyoainishwa na wahusika wakamatwe.
Ifuatayo ni ripoti kamili ya uchunguzi:
Utangulizi:
Usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, 2013,
Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, ambaye pia Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alivamiwa na
kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake Mbezi
Juu, Dar es Salaam.
Tukio hilo lilishtua na kutikisa taifa kwa kiwango kikubwa si tu katika tasnia ya habari nchini, bali pia jamii kwa jumla hasa baada ya aina ya utekaji, utesaji na usiri uliotumika katika kufanikisha uhalifu huu kufanana kwa karibu na tukio lililomkuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka lililotokea karibu miezi tisa kabla ya tukio la Kibanda yaani, usiku wa Juni 26, 2012.
Ukiacha matukio hayo, miezi sita kabla ya Kibanda kutekwa na kuteswa Mwandishi Daudi Mwangosi, aliuawa akiwa mikononi mwa vyombo vya dola Septemba 2, 2012 huko Nyololo, Iringa akiwa kazini.
Tukio la Kibanda limekuwa na sura ya mwendelezo wa
mauaji au utesaji wa wanahabari, hasa ikitiliwa maanani kuwa Mwandishi
Issa Ngumba (45) wa Radio Kwizera aliyekuwa anafanyia kazi zake katika
Wilaya ya Kakonko, Kigoma, Januari mwaka huu, alipigwa risasi na kuuawa
katika mazingira ya kutatanisha.
Mazingira ya kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda yalitia wasiwasi kuwa upo uwezekano na dalili zilionyesha kwamba waliofanya kitendo hicho cha kinyama hawakuwa wezi wala majambazi kutokana na ukweli kwamba licha ya kuwa na fedha zipatazo shilingi milioni tatu taslimu ndani ya gari, laptop, simu tatu za gharama (ipad, iphone na Blackberry), watekaji hawa hawakuchukua chochote baada ya kukamilisha uhalifu wao.
Kibanda aliumizwa kwa kiwango kikubwa. Alitobolewa jicho la kushoto, akaumizwa vibaya kichwani kiasi cha kusababisha kuvunjika kwa baadhi ya mifupa ya kichwa. Aling’olewa meno mawili na kucha mbili, tena bila ganzi. Watekaji hawa, katika unyama wa ajabu kabisa, walimkata pingiri ya kidole cha pete chini ya kucha na kuondokana nayo.
Hali hiyo iliibua maswali mengi, watu wengi wakajiuliza na kutafuta sababu za kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda kiasi hiki. Kutokana na kuwapo kwa maelezo mengi yanayotofautiana kuhusu tukio hilo, ikabidi Jukwaa la Wahariri Tanzania lifanye uamuzi.
Timu hiyo iliundwa kutokana na uamuzi wa Jukwaa la Wahariri kufanya uchunguzi huo na baada ya kukubalika kwa ombi la ruzuku ya kufanya uchunguzi huo wa kihabari kutoka Mfuko wa Vyombo
Vya Habari Tanzania (TMF).
Timu hii imefanya kazi usiku na mchana kwa zaidi ya mwezi. Timu imezungumza na wadau 26. Kati ya hawa yumo Kibanda mwenyewe, mke wake, ndugu zake, wasaidizi wake, waajiri wake wa zamani na wa sasa, viongozi wa kisiasa na vyombo vya dola kutafuta ukweli wa jambo hili. Pia tumesoma matamko na habari zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ya kati ya Machi 5, 2012 na Aprili 5, 2012 kwa nia ya kufanya ulinganishi wa taarifa tulizozipata kutokana na uchunguzi na habari zilizochapishwa baada ya kutekwa kwake.
Vyombo vya dola akiwamo Waziri mwenye dhamana walikataa kuhojiwa wakisema kuna tume ya Serikali inayofanya kazi hiyo na kwamba kuhojiwa kungeonyesha kutokuwa na imani na tume hiyo.
Kama hiyo haitoshi, tukio la kutekwa na kudhuriwa kwa Kibanda
limetokea mwezi mmoja tu baada ya Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima,
Shaaban Matutu kupigwa risasi na polisi akiwa nyumbani kwake Dar es
Salaam kwa maelezo ilikuwa kimakosa polisi walidhani Matutu ni jambazi.
Mazingira ya kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda yalitia wasiwasi kuwa upo uwezekano na dalili zilionyesha kwamba waliofanya kitendo hicho cha kinyama hawakuwa wezi wala majambazi kutokana na ukweli kwamba licha ya kuwa na fedha zipatazo shilingi milioni tatu taslimu ndani ya gari, laptop, simu tatu za gharama (ipad, iphone na Blackberry), watekaji hawa hawakuchukua chochote baada ya kukamilisha uhalifu wao.
Kibanda aliumizwa kwa kiwango kikubwa. Alitobolewa jicho la kushoto, akaumizwa vibaya kichwani kiasi cha kusababisha kuvunjika kwa baadhi ya mifupa ya kichwa. Aling’olewa meno mawili na kucha mbili, tena bila ganzi. Watekaji hawa, katika unyama wa ajabu kabisa, walimkata pingiri ya kidole cha pete chini ya kucha na kuondokana nayo.
Hali hiyo iliibua maswali mengi, watu wengi wakajiuliza na kutafuta sababu za kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda kiasi hiki. Kutokana na kuwapo kwa maelezo mengi yanayotofautiana kuhusu tukio hilo, ikabidi Jukwaa la Wahariri Tanzania lifanye uamuzi.
Katika kikao cha Machi 8, 2013 Jukwaa la Wahariri
Tanzania liliunda TIMU ya watu watano na kuipa hadidu rejea za kufanya
uchunguzi wa kihabari juu ya shambulio hilo kubaini limetokana na nini.
Timu hiyo iliundwa kutokana na uamuzi wa Jukwaa la Wahariri kufanya uchunguzi huo na baada ya kukubalika kwa ombi la ruzuku ya kufanya uchunguzi huo wa kihabari kutoka Mfuko wa Vyombo
Vya Habari Tanzania (TMF).
Ruzuku ya TMF ililenga kiujumla kutumia tukio la
Kibanda kuwa chanzo cha kutengeneza mazingira salama zaidi kwa waandishi
na wahariri na kwamba kiwango cha matukio ya kuteswa, kupigwa na kuuawa
kwa waandishi yanapungua kila mwaka.
Timu hii imefanya kazi usiku na mchana kwa zaidi ya mwezi. Timu imezungumza na wadau 26. Kati ya hawa yumo Kibanda mwenyewe, mke wake, ndugu zake, wasaidizi wake, waajiri wake wa zamani na wa sasa, viongozi wa kisiasa na vyombo vya dola kutafuta ukweli wa jambo hili. Pia tumesoma matamko na habari zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ya kati ya Machi 5, 2012 na Aprili 5, 2012 kwa nia ya kufanya ulinganishi wa taarifa tulizozipata kutokana na uchunguzi na habari zilizochapishwa baada ya kutekwa kwake.
Vyombo vya dola akiwamo Waziri mwenye dhamana walikataa kuhojiwa wakisema kuna tume ya Serikali inayofanya kazi hiyo na kwamba kuhojiwa kungeonyesha kutokuwa na imani na tume hiyo.
Leo tunawasilisha muhtasari wa ripoti hii. Ripoti
kubwa pamoja na viambatanisho vyake, itachapishwa na kuwekwa katika
kitabu kimoja. Utaratibu mwingine wa kuchapisha habari ambazo
hazijachapishwa kuhusiana na tukio hili (untold stories) pia utaandaliwa
kwa ushirikiano na Jukwaa la Wahariri kwa nia ya kuieleza jamii maajabu
juu ya kadhia hii.
Tulipewa Hadidu Rejea ziafuatazo:-
Hadidu rejea:
Kuchunguza mazingira ya kabla na baada ya tukio la
kushambuliwa kwake. Kabla ya kushambuliwa kwa maana ya kufahamu kama
kulikuwa na viashiria vyovyote vinavyoelekea kuwapo kwa mipango ya
mashambulizi dhidi yake.
Kuchunguza mazingira ya tukio lenyewe kwa kujikita katika mwenendo wake hasa siku nzima ya Jumanne Machi 5, 2013.
Kuangalia mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya
New Habari (2006), Ltd na nje ya kampuni hiyo kwa kumulika sababu za
kuhama kwake kutoka Free Media mwishoni mwa mwaka jana na kuhamia New
Habari.
Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.
Kuchunguza mazingira ya sasa ya kazi kwa wanahabari na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kile kitakachobainika.
Yaliyojiri katika uchunguzi:
Kuchunguza mazingira ya kabla na baada ya tukio la
kushambuliwa kwake. Kabla ya kushambuliwa kwa maana ya kufahamu kama
kulikuwa na viashiria vyovyote vinavyoelekea kuwapo kwa mipango ya
mashambulizi dhidi yake.
Timu ya uchunguzi ilitumia muda mwingi katika eneo
hili, kubaini iwapo kulikuwapo viashiria, sababu au matukio ya wazi
yenye mwelekeo wa kujitokeza kwa shambulio hili. Tuliangalia pia iwapo
wapo watu au makundi yaliyokwishapata kuonyesha ishara kwa matendo au
kwa kauli juu ya uwapo wa nia hii.
Uchunguzi umebaini kuwa kuliwapo viashiria vingi,
isipokuwa Kibanda au watu wake wa karibu hawakupata kufikiri kuwa huenda
vingeweza kuleta madhara makubwa kiasi hiki kama ifuatayo:-
1.1. Wiki tatu kabla ya Kibanda kuvamiwa, kutekwa
na kuumizwa, gari la polisi aina ya gofu Na PT 180 liliwafuatilia kwa
muda mrefu Absalom Kibanda na Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006)
Ltd, Hussein Bashe likiwa limeegeshwa nje ya ofisi zao Sinza Kijiweni
na baadaye likawafuatilia hadi Sinza Makaburini, ambapo
walisimamisha magari yao na kuzungumza na polisi hao waliosema walikuwa
wanatilia shaka magari yao. Baada ya kuzungumza kwa muda polisi
waliondoka.
1.2. Usiku wa Februari 25, mwaka huu majira ya saa
9:00 usiku, Kibanda alivamiwa na watu walioingia kwenye uzio wa nyumba
yao wakavunja kioo cha gari analotumia, lakini kioo kilipovunjwa ‘alarm’
ilipiga kelele, Kibanda akatoka nje na watu hao wakakimbia.
1.3. Kutokana na uvamizi huo, Kibanda na wapangaji
wengine katika nyumba zilizopo kwenye uzio mmoja, waliona hatari ya
kuvamiwa hivyo wakaanza mazungumzo na kampuni ya Ulinzi ya Kiwango,
iliyowataka kufunga kamera za usalama na kuweka walinzi watano. Hadi
Kibanda anatekwa, walikuwa hawajahitimisha mazungumzo na kampuni hii ya
Kiwango.
1.4. Kuna askari anayefanya kazi Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) miezi minane kabla alipata kumpa Kibanda taarifa za
kintelijensia.
Inaendelea kesho
kuwa kulikuwapo mpango wa kumteka na kumuumiza.
Taarifa kama hizo pia alipewa na wasamaria wanaofanya kazi katika Jeshi
la Polisi. Kwa maneno yake Kibanda alisema:
“Kuna rafiki yangu askari wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), kama miezi minane au tisa hivi aliwahi kuniambia
‘unaandika sana usidhani kama watu wanakupenda. Chukua tahadhari hasa
unapofika getini nyumbani kwako’. Tangu wakati huo nimekuwa nikichukua
tahadhari sana.
“Wiki mbili kabla ya tukio, niliwahi kuhisi kitu
kama hicho [cha kuvamiwa] nikiwa getini. Nilipiga honi wakachelewa kuja
kunifungulia, niliogopa sana. Hata nilipoingia ndani nilikuwa nimekosa
raha kabisa.
“Pia kuna rafiki zangu polisi waliwahi kuniambia
kwamba ninatafutwa na kwamba watu wananifuatilia na ikibidi
wanitengenezee ajali au kunifanyia kama Ulimboka au Kubenea.”
1.5. Ndani ya miezi mitatu mbele ya mlango wa
ofisi yake Kibanda (Free Media Limited) ilikuwa mara kwa mara muda wa
asubuhi anapofika ofisini anakuta damu. Haikufahamika kama damu hiyo
ilikuwa ni ya binadamu, kuku, ng’ombe, kunguru au mbuzi, bali waliipuuza
wakidhani ni masuala ya ushirikina. Mhariri Mtendaji wa sasa,
Inaendelea kesho
Ansbert Ngurumo, amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo.
1.6. Mfanyakazi mwandamizi wa Kampuni ya New
Habari anakofanya kazi sasa Kibanda ndani ya wiki mbili kabla ya kutekwa
na kuumizwa kwake alipata kumwabia Kibanda maneno mazito mara tatu, na
hapa tunamnukuhu Kibanda:
“Aliniambia Danny Mwakiteleko [aliyekuwa Naibu
Mhariri Mtendaji wa New Habari] hakufa kwa ajali, bali alikufa kutokana
na blood clotting (kuganda kwa damu). Hivyo ikitokea mtu ukapata ajali
au ukapigwa na kuumizwa sana sehemu za kichwa hivi au tumbo, ni lazima
madaktari wadhibiti sana blood clotting.
“Na kweli, nilivyoletwa hapa Milpark hospitalini,
madaktari walikuwa wananidunga sindano sita kila siku kwenye kitovu
kuzuia blood clotting. .... (jina linahifadhiwa) aliniambia maneno haya
mara tatu, katika mazingira yasiliyotarajiwa na kwa msisitizo ambao
sikujua maana yake. Nasema .... (jina linahifadhiwa) naye achunguzwe kwa
kina. Inawezekana kuna jambo analijua.”
Ofisa huyu, alipishana dakika chache na Kibanda
muda wa kutoka ofisini baada ya kipindi cha kwanza cha mechi kati ya
Real Madrid na Manchester united kumaliza nusu ya kwanza (half time).
Dakika ishirini baadaye Kibanda alishambuliwa.
Kuchunguza mazingira ya tukio lenyewe kwa kujikitika katika mwenendo wake hasa siku nzima ya Jumanne Machi 5, 2013.
2.1. Familia ya Kibanda na Kibanda Mwenyewe
hawakuwa na wasiwasi wowote siku hiyo kwani hawakuwa na hisia wala wazo
kuwa ungetokea uvamizi huo.
2.2. Kibanda alipopiga honi, mlinzi alisogea
langoni kumfungulia. Ghafla akasikia kishindo kikubwa. Akasikia kelele
za Kibanda akiomba msaada. Kijana huyu Baraka Ibrahim mwenye umri wa
miaka 27, aliogopa. Aliogopa kwa mana hakuwa na silaha yoyote mkononi.
Hakuwa na panga, kisu, rungu, wala filimbi. Kwa maneno yake anasema:
“Nilivyoona ningefungua geti hata mimi ningekufa,
nilikimbia kuwaamsha majirani. Sikuwa hata na namba ya simu ya mtu
yeyote kati ya mabosi wangu ninaowalinda. Nilikuwa mimi tu, imani yangu
na Mungu wangu.... kutokana na maisha naifanya hivyo hivyo tu.
Vinginevyo milele nisingefanya kazi hii ya ulinzi.”
Mlinzi huyo alikimbilia kwa majirani katika nyumba
aliyoamini yumo mwanaume, lakini akaanza kumwamsha House Girl, ili
house girl amwamshe baba mwenyenyumba. Kitendo cha kuamshana na kuwapa
taarifa kilichukua dakika tano hadi saba, na ndani ya muda huo, Mlinzi
anasema watekaji wa Kibanda walifanyafanya unyama na uasi huo na
kuondoka ndani ya muda mfupi kiasi hicho. “Watu hawa wana mafunzo
maalumu,” anahitimisha.
2.3. Mke wake alikwenda kazini asubuhi na kurejea
nyumbani jioni, lakini tofauti na utaratibu wake wa kawaida ambapo huwa
anaangalia televisheni sebuleni hadi Kibanda anaporejea nyumbani, siku
hiyo alikwenda kuangalia televisheni akiwa chumbani na usingizi
ukampitia. Anasema hakusikia honi wala tukio la Kibanda kutekwa. “Hii
inanitesa sana moyoni. Najiuliza kwa nini siku hiyo tu sikukaa sebuleni?
Kwa nini siku hiyo tu nimelala mapema kabla Baba Joshua hajarudi
(machozi yanamlengalenga). Najiuliza sipati jibu.”
2.4. Mmoja kati ya wasaidizi wawili wa nyumbani kwa Kibanda,
alisikia kelele za Kibanda akiomba msaada. Alimwamsha mwenzake na
kumwambia. “Nasikia Baba Joshua anapiga kelele kama amevamiwa hivi.”
Mwenzake alimwambia “Unaota maana kuna kelele za mpira.” Siku hiyo
kulikuwa na mechi kati ya Real Madrid na Manchester United.
Ni kweli zilikuwapo pia kelele za wanaoshangilia
mpira siku hiyo, hivyo Kibanda alipoomba msaada, hata waliosikia
walidhani watu wanashangilia mpira. Binti aliwaamsha Angela na mwenzake,
wakaenda sebuleni, wakakaa na kuchungulia dirishani, wakaona mwanga wa
gari getini, lakini baada ya kutosikia kelele yoyote wakarejea kulala
wakidhani siye. Lakini binti mmoja alibaki sebuleni. Baada ya muda
jirani mmoja akampigia simu Angela kumweleza kuwa mumewe ameshambuliwa.
2.5. Kibanda kwa upande wake, anasema alipofika
getini, alipiga honi, ghafla akaona watu wawili wamesimama pembeni mwa
gari lake na mtu wa tatu akiwa kwa mbali. Kisha akasikia kishindo
kikubwa, akidhani wanataka kuiba gari, aliatokea mlango wa abiria na
kuanza kukimbia huku akiita. “Mama Joshua nisaidieeeeee.”
Katika kukimbia, aliteleza akaanguka. Huku
watesaji wake wakisema mara tatu “Afande piga risasi.” Kibanda alijaribu
kupambana, akashika rungu, akawahoji amewakosea nini hadi wampige kiasi
hicho, lakini hawakumjibu lolote. Waliendelea kumpiga, hadi akapoteza
fahamu. Hakujua jicho limetobolewa saa ngapi, meno yameng’olewaje na
wala pingiri ya kidole chake imekatawaje. Ifuatayo ni sauti ya Kibanda
mwenyewe. Inasikitisha ila tuwe wavumilivu na tuisikilize.
Kuangalia mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya
New Habari (2006) Ltd na nje ya kampuni hiyo kwa kumulika sababu za
kuhama kwake kutoka Free Media mwishoni mwa mwaka jana na kuhamia New
Habari.
3.1. Mazingira ya kazi ndani ya New Habari (2006)
Limited na Freemedia Limited, yanaacha maswali kadhaa yenye kustahili
majibu. Kama ilivyoelezwa kwenye Hadidu Rejea Na: 1, ndani ya kampuni ya
New Habari imekuwapo misuguano isiyo na afya kwa kazi ya Kibanda kama
mwandishi na tasnia ya habari kwa ujumla.
3.2. Mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd
ni utata. Uhusiano katika chumba cha habari si mzuri. Ndani ya kampuni
hawaaminiani na imefikia hatua wanatuhumiana kuwa huenda baadhi ya
viongozi ndani ya New Habari wamehusika kumteka na kumuumiza Kibanda.
Haya yameandikwa ndani ya mitandao ya kijamii, ikidai kwamba kiongozi
mmoja ndani ya kampuni hiyo alihusika na utekaji wa Kibanda.
Mkurugenzi wa Uhariri, Prince Bagenda anasema
waliohusika kusambaza taarifa chafu dhidi ya kiongozi huyo wa New Habari
wanatoka ndani ya kampuni hiyo.
3.3. Timu ya uchunguzi ilibaini kuwapo mgawanyiko
mkubwa ndani ya New Habari (2006) Ltd kwa kuwapo kundi la ‘Habari
Wazawa’ na ‘Habari wa Kuja’. Malalamiko mengi yanajikita katika msingi
kuwa ajira hazitangazwi na watu wanaajiriwa bila kuzingatia sifa za
kitaaluma.
3.4. Kibanda hakuhama Free Media kwa amani.
Uchunguzi unaonyesha kuwa miezi kadhaa kabla ya kuondoka kwake alianza
kupoteza mamlaka. Mwenyekiti wa Kampuni ya Free Media Ltd, Freeman Mbowe
alianza kumsikiliza zaidi msaidizi wake ambaye alikuwa Naibu Mhariri
Mtendaji, Ansbert Ngurumo kuliko yeye Kibanda. Kwa maneno yake, anasema:
“Nilihofu kuwa Mbowe anaweza kutugombanisha. Nikaona ni bora niondoke nisije nikagombana na Mbowe au Ngurumo.”
Anasema alianza kupoteza mamlaka yake na
kutoaminika kwa mwajiri wake baada ya kuandika makala kuhusu Abdulrahman
Kinana ambayo kabla ya kuiandika hakuwa na wazo la kuondoka.
Yaliyofuata baada ya makala hiyo, yalimshukuma aondoke.
Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.
4.1. Uchunguzi ulifuatilia masuala mbalimbali
ikiwamo miendendo ya watu waliotajwa kwa njia moja au nyingine kuhusinaa
na tukio hili. Hata hivyo, karibu watu wote waliohojiwa, akiwamo
Kibanda mwenyewe aliyeumizwa walimtaja kwa kutilia shaka mwenendo wa
kijana Joseph Ludovick. Hofu yao, iliongezwa nguvu na maandishi
aliyoyachapisha Ludovick kwenye mitandano ya kijamii siku ya Machi 6,
2013.
4.2. Usiku aliotekwa na kuumizwa Kibanda, Ludovick katika naye
alidai kuwa ametekwa katika eneo la Shekilango na kupelekwa hadi Kigogo.
Baada ya kutekwa aliibiwa kila kitu, ikiwamo begi, laptop, simu mbili,
fedha taslimu Sh 35,000, akavuliwa nguo na kubaki na chupi tu. Pia
alieleza kuwa alitoa taarifa hizo kituo cha polisi Mabibo.
4.3. Maelezo ya Ludovick yalitiliwa shaka na watu
wengi hasa baada ya kuleeza kuwa watekaji walitumia muda wa saa mbili
kumtoa Shekilango hadi Mabibo, umbali ambao kwa kiwaida mwendo wake
hauwezi kuzidi dakika 10.
4.4. Daniel Chongolo aliiambia timu kuwa alfajiri
ya Machi 6, siku anayodai kutekwa Ludovick yeye alimuona eneo la Mabibo
wakati anatoka Muhimbili. Chongolo alikwenda kituo cha polisi Mabibo na
kupewa taarifa kuwa Ludovick alitoa taarifa polisi kuwa alikuwa ametekwa
ila akarudishiwa mali zake zote.
“Alipouliza amefuata nini polisi, akawambia kama
raia mwema amefika kuandikisha kumbukumbu kwa nia ya kuonyesha kiwango
cha uhalifu kinavyoongezeka nchini,” anasema Chongolo. Timu ya uchunguzi
ilikataliwa kupitia leja ya polisi kama itakavyoelezwa hapa chini.
4.5. Pia taarifa za uchunguzi wa timu hii
zinathibitisha kuwapo kwa utata juu ya madai ya kuibwa kwa simu za
Joseph Ludovick, kwani simu yake ya tigo (inayodaiwa kuibwa) ilitumika
saa 01:21 asubuhi siku ya Machi 6, 2013. Muda huu ofisi za Serikali na
Kampuni ya Tigo zilikuwa hazijafunguliwa
Kuchunguza mazingira ya sasa ya kazi kwa wanahabari na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kile kitakachobainika.
5.1. Uchunguzi umebaini kuwa maisha ya wanahabari
yapo hatarini. Hatari hii inatokana na makundi mengi yenye masilahi
kuwaona wanahabari wanaosimamia ukweli kuwa maadui wa masilahi yao
haramu. Kuna hatari kubwa inayowakabili waandishi wakati nchi
inapoelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
5.2. Uchunguzi umebaini kuwa usiri umepungua katika vyombo vya
habari. Tofauti na zamani ambapo habari nyeti ziliandikwa kwa kuhifadhi
majina ya waandishi wakitumia jina la MWANDISHI WETU. Simu hizi hata
habari za kutisha waandishi wanaweka majina yao na hata wasipoweka,
ndani ya vyumba vya habari vingi waandishi wapo tayari kutaja nani
ameandika habari fulani.
5.3. Usaliti miongoni mwa waandishi wenyewe ndani
ya vyumba vya habari unazidi kuongezeka na usipodhibitiwa hali itazidi
kuwa mbaya zaidi. Mwenyekiti wa MOAT, Dk. Reginald Mengi anasema: “Hili
ni jambo muhimu sana. Tuache usaliti vinginevyo wengi wataumia.”
5.4. Pia alishauri waandishi wa habari kurejea
katika msingi wa taaluma, ambayo inawataka wao kuwa ndio wenye kuendesha
vyombo vya habari badala ya kutegemea matakwa ya wamiliki au makundi
yenye masilahi binafsi.
KILICHOBAINIKA:
6.1. Uchambuzi uliofanywa ni timu hii umebaini
kuwa hoja nne zinazungumzwa kuhusiana na kutekwa na kuumizwa kwa
Kibanda. Hoja hizi ni:-
(i) Kazi yake ya uandishi wa habari
(ii) Uhusiano wa kisiasa na vyama au wanasiasa mbalimbali
(iii)Uhusiano wa kijamii ikiwamo mapenzi
6.6. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anadai
kwamba mpango kama huo vyombo vya dola viliutumia kwa NCCR Mageuzi
vikakisambaratisha, Chama cha Wananchi (CUF) kilisingiziwa udini
kikapoteza mwelekeo na sasa vyombo hivyo vililenga kukifanya CHADEMA
kionekane cha kigaidi mbele ya macho ya jamii ndiyo maana imerekodiwa
mikanda kwa nia ya kuitumia kujenga hoja hiyo
(iv) Vitendo vya rushwa.
6.2. Timu imejiridhisha kutokana na majibu ya
wengi kuwa dhana ya mapenzi na rushwa, havina nafasi yoyote katika tukio
hili. Wote waliohojiwa walieleza pasi na shaka kwamba suala hili la
kushambuliwa na kuumizwa kwa kiwango kikubwa kwa Kibanda, halina
uhusiano wowote na rushwa au mapenzi.
6.3. Kutokana na yaliyotajwa hapo juu kazi yake na
siasa vikiunganishwa vimechangia kwa kiasi kikubwa kuvamiwa kwa
Kibanda. Timu imebaini kuwa kuna kutupiana mpira kati ya vyombo vya dola
na vyama vya siasa. Mchezo huu mchafu unaweza ukawa mwanzo wa kuumizwa
kwa Kibanda na waandishin wengine.
6.4. Baadhi ya waliohojiwa walidai kuwa utekaji
huu umefanywa na vyombo vya dola ukiwa sehemu ya mpango mkakati wa
vyombo hivi kukihusisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na
vitendo vya ugaidi.
6.5. Wanayataja matukio ya Uchaguzi Mdogo wa
Igunga, maandamano ya Morogoro na Mkanda anaodaiwa kurekodiwa Mkurugenzi
wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare kuwa vililenga kukifanya
CHADEMA kichukiwe na Watanzania kwa kukitaja kama chama cha kigaidi
ambacho kinateka watu na kinawaumiza.
6.7. Wakati Mbowe akisema hayo, baadhi ya watu waliohojiwa
wanadai kuwa CHADEMA kimepewa mafunzo na ushauri kutoka nje ya nchi kuwa
kikitumia baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola wasiokuwa waaminifu
kuteka, kuumiza na hata kuua baadhi ya watu maarufu nchini wakiwamo
waandishi na wanasiasa, basi wananchi wataamini kuwa Chama Cha Mapinduzi
na Serikali yake kimeshindwa uongozi na sasa kimeanza kazi ya kuua
wanaowapinga.
6.8. Kwa njia hiyo, inaelezwa kuwa hesabu za
Chadema ni kuwa wananchi wataichukia CCM na Serikali yake na kukipa
nafasi ya kuingia madarakani. Hapa kauli ya Chadema kuwa NCHI
HAITATAWALIKA itakuwa imetimia.
6.9. Dhana nyingine iliyojitokeza ni kuwa wapo
wafanyabiashara ambao wana vita binafsi, hivyo wanaamua kuumiza watu
wasiowaunga mkono katika mipango yao na hilo ndilo limemkumba Kibanda,
baada ya kuwa ameepusha mauaji ya mwandishi mmoja na aliyekuwa ameandaa
mpango wa kuua mwandishi huyo hakuridhika hivyo akaamua amshughulikie
Kibanda.
MAPENDEKEZO:
Baada ya Timu kupata taarifa hizi na nyingine nyingi, inapendekeza yafuatayo:-
7.1. Taarifa hii ichukuliwe kama chanzo cha uchunguzi zaidi wa vyombo husika.
7.2. Yanahitajika marekebisho makubwa na ya haraka
katika mifumo ya uendeshaji wa vyumba vya habari kwa nia ya kurejesha
misingi ya uandishi wa habari inayokubalika.
7.3. Usalama wa wanahabari unapaswa kupewa
kipaumbele na wamiliki, wanahabari wenyewe na jamii kwa ujumla. Hapa
Timu inapendekeza yawepo mafunzo ya kuwawezesha wanahabari kutambua
viashiria vya hatari na kuchukua hatua mara moja.
7.4. Kwa kiwango alichoumizwa Kibanda iwapo mwajiri wake
asingejitolea kugharamia matibabu, hatujui hatima yake ingekuwaje leo
hii. Tunapendekeza taasisi na mifuko mbalimbali inayojihusisha na
masuala ya wanahabari kama Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) , Baraza la
Habari Tanzania (MCT), Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) na
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kuanzisha mfuko wa
pamoja utakaotumika kugharamia matibabu ya waandishi watakaoumia wakiwa
kazini.
7.5. Tukio la kutekwa kwa Kibanda limeonyesha
mwanga kuwa wahariri tumegawanyika mno. Habari zilizochapishwa katika
magazeti mbalimbali na mitandao ya kijamii zimeonyesha haja ya kuwafanya
wahariri kuwa kitu kimoja kwa kuondoa tofauti zao zisizo na masilahi
kwa tasnia ya habari.
7.6. Kuna viashiria vingi kuwa kuelekea mwaka 2015
matukio ya waandishi kuumizwa au kutekwa yanaweza kuongezeka kutokana
na wanasiasa na vyama kuwania madaraka huku wakitumia baadhi ya
watumishi katika vyombo vya dola. Kwa mantiki hiyo, vyombo vya habari na
waandishi wa habari wachukue tahadhari kuanzia sasa.
7.7. Taasisi za habari zifanye juhudi za makusudi
kukutana na vyama viwili vya siasa vya CCM na CHADEMA haraka
iwezekanavyo, kuzungumzia viashiria hivi vya hatari vinavyoelekea
kuvuruga amani ya Tanzania.
HITIMISHO:
Ni dhahiri kuwa kupigwa na kuteswa kwa Kibanda
kumejiegemeza katika siasa na kazi yake, hali inayofanya makundi muhimu
kuchukua wajibu wa msingi. Kwa upande wa Serikali ni muhimu kufuatilia
viashiria katika taarifa hii kwa nia ya kupata ukweli zaidi na kuchukua
hatua stahiki za kisheria dhidi ya wahusika.
Na kwa upande wa vyombo vya habari na taasisi za
kihabari zinapaswa kutambua viashiria vinavyohatarisha usalama wa
waandishi wa habari na wahariri na kutengeneza mazingira yatayokuwa
salama zaidi kwa waandishi kufanya kazi zao.
SHUKRANI:
9.1. Tunapenda kulishukuru Jukwaa la Wahariri Tanzania, kwa
kufanya uamuzi sahihi wa kuwezesha kufanyika kwa uchunguzi huu ulioanza
kuonyesha mwanga wa nini kilitokea.
9.2. Tunapenda kulishukuru Baraza la Habari
Tanzania (MCT) kwa kushiriki kikamilifu na kuiwezesha timu hii kwa
Rasilimali Watu na Mali kufanikisha kazi hii.
9.3. Tunapenda kuwashukuru Mfuko wa Vyombo vya
Habari Tanzania (TMF) kwa uwezeshaji wa ruzuku, uliofanikisha kufanya
uchunguzi wa kihabari uliohusisha kwenda nchini Afrika Kusini kufanya
mahojiano na Kibanda. Uwezeshaji huo pia unahusisha kutengeneza mwongozo
kwa waandishi wenye lengo la kuwaepusha na hatari za kiusalama.
9.4. Tunawashukuru Kibanda, mkewe Angela,
wanafamilia, ndugu na jamaa wa Kibanda na wanahabari wote waliohojiwa
kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Timu hii.
9.5. Tunawashukuru wahariri wote kila mtu kwa
nafasi yake, kutokana na ushauri wa mara kwa mara mliotupatia katika
kufanikisha uchunguzi huu.
WAJUMBE WA TIMU:
Timu hii iliundwa na wajumbe watano ambalo ni:
Deodatus Balile – Mwenyekiti
Pili Mtambalike – Mjumbe
Jane Mihanji – Mjumbe
Tumaini Mwailenge – Mjumbe
Rashid Kejo – Katibu
No comments:
Post a Comment