
Ofisi za Gaeti la Daily Monitor zilizovamiwa na polisi wa Uganda
Polisi nchini Ugandan wamevamia
ofisi za magazeti kufuatia taarifa kwamba Rais Yeweri Museveni
anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi urais.
Vituo viwili vya Redio pia vamiwa na kuzimwa , hii ni kwa muujibu wa gazeti la serikali la New Vision.
Wiki iliyopita magazeti ya Uganda
yalidai kuwa kuna njama za kuwaua wale watakao pinga mpango wa Rais
Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya Uganda.
Magazeti hayo yalidai kuwa mipango hiyo ya mauaji yalitolewa na Mkuu fulani wa jeshi la Uganda.
Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anatarajiwa kung'atuka uongozini mwaka 2016.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kwamba Museveni
anamuandaa mwanawe Muhoozi Kainerugaba,ambaye ni brigadier jeshini
kushikilia uongozi wa Uganda.
Lakini serikali ya Museveni imekanusha kwamba kuna mipango kama hiyo.
Mwanawe Museveni Brig. Kainerugaba.
Wiki iliyopita gazeti la, the Daily Monitor,na
jengine la , Red Pepper, lilichapisha barua ya siri ikidai ilikuwa
imeandikwa na Jeneral David Sejusa, ikitaka uchunguzi ufanywe
kuthibitisha madai kwamba kuna mipango ya kuwauwa wote watakao piga
mipango ya Rais Museveni kumpachika mwanawe uongozini.
Uvamizi huo wa polisi umeidhinishwa na mahakama
ya Uganda na ulikuwa unalengo la kutafuta barua hiyo inayodaiwa
kuandikwa na mkuu huyo wa Jeshi akifichua njama za mauaji.
Vituo viwili vya Redio vinavyohusiana na Daily Monitor, Dembe FM na KFM, pia vilivamiwa na kuzimwa.

Rais Yoweri Museveni
Mkurugenzi Mkuu wa Daily Monitor Bwana Alex
Assimwe aliambia BBC kwamba Chumba chao cha Habari kilivamiwa na polisi
wapatao 50 waliojihami kwa silaha.
Lakini wachanganuzi wa maswala ya kisiasa
wanadai kuwa ikiwa barua ya Jenerali Sejusa ni ya kweli basi ni dalili
kuwa kuna hali mvutano ndani ya jeshi huku ikidhaniwa kuwa wanajeshi
wakongwe huenda wanapoteza uwezo kwa wanajeshi chipukizi wanaoongozwa na
mwanawe Museveni Brigadia Kainerugaba.
Jenerali Sejusa ni mwanajeshi mkongwe aliyekuwa katika vita vya ukombozi uliyomuweka Rais Museveni madarakani mwaka1986.
Kwa muujibu wa taarifa za AP kamanda mmoja wa
jeshi Jenerali Aronda Nyakairima amenukiliwa akisema kuwa Jenerali
Sejusa kwa wakati huu anachunguzwa kutokana na barua anayodaiwa
kuiandika.
No comments:
Post a Comment