Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kulia) akimkabidhi fulana mwanafunzi wa Chuo cha TIA Mkoani Mbeya,Steven Kiasi kwa ajili ya mashindano ya Safari Lager Pool |
Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kulia) akimkabidhi fulana mwanafunzi wa Chuo cha MUST Mkoani Mbeya,Mwita Masasi kwa ajili ya mashindano ya Safari Lager Pool |
Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kulia) akimkabidhi fulana mwanafunzi wa Chuo cha TEK Mkoani Mbeya,Msuda Jeremia kwa ajili ya mashindano ya Safari Lager Pool |
MASHINDANO
ya mchezo wa Pool Table kwa vyuo vikuu mkoani Mbeya yanafanyika leo kwenye
Viwanja vya CCM Iloma
Jumla ya Vyuo
vikuu vinne vilivyopo Mbeya vitashiriki ambavyo ni ni Mzumbe tawi la Mbeya,
Chuo cha Uhasibu (TIA), Chuo cha Ufundi (TEK) na MUST na vimeshakabidhiwa vifaa vya mashindano.
Akizungumza kwa njia ya Simu toka Mbeya,
Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Pool mkoa wa Mbeya(MRPA), Aron Samweli
amesema kuwa mashindano hayo yatakayoshirikisha vyuo vikuu vinne ambavyo ni
Mzumbe tawi la Mbeya, Chuo cha Uhasibu Mbeya, Chuo cha Ufundi na MUST.
“Mashindano
ya pool yataanza kesho na vyuo vikuu vya Mzumbe tawi la Mbeya, Chuo cha Uhasibu
Mbeya, Chuo cha Ufundi na MUST ndio vitakavyoshiriki na vimeshachukuwa vifaa
vya mashindano “, alisema Samweli
Pia amesema
chuo kitakachobeba ubingwa wa mkoa huo ndicho kitakacho shiriki katika fainali
za taifa za mashindano hayo zitakazofanyika Juni mosi, mwaka huu jijini Dar es
salaam.
Bingwa wa
mashindano hayo kwa upande wa timu katika ngazi ya mkoa atajinyakulia fedha
taslim Sh.500,000, mshindi wa pili Sh.300,000, mshindi wa tatu Sh.200,000 na
mshindi wa nne Sh.100,000.
No comments:
Post a Comment