WATOTO watano waliozaliwa kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Ruvuma kwa wakati mmoja wamefariki dunia.
Aliyewazaa watoto
hao ni Sophia Mgaya (28) mkazi wa Ruhuwiko Manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma. Watoto hao waliishi kwa saa 10 tu.
Mama yao ni mwajiriwa mpya wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi katika shule ya sekondari
Luhawasi mjini Songea.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Benedict Ngaiza alisema watoto hao watano walizaliwa baada ya miezi minane.
Alisema watoto hao walikuwa wakiendelea vizuri ingawa wote walikuwa na uzito mdogo huku mwenye uzito mkubwa akiwa na gramu 820 na mwenye uzito mdogo akiwa na gramu 430.
Dk. Ngaiza alisema kitendo cha kuzaliwa kabla ya muda stahili kimechangia watoto hao kufariki dunia.
Watoto hao walizikwa katika makaburi ya Lilambo mjini Songea.

No comments:
Post a Comment