MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sofia Simba, amewataka
wanafunzi wa elimu ya juu kukataa kurubuniwa na watu wachache ambao
hawaitakii mema Tanzania.
Kauli hiyo aliitoa mjini hapa juzi wakati
alipozindua Mpango Kazi wa Kitaifa kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ambapo
wameanza na vyuo vikuu vilivyopo Dodoma.
Alisema kumekuwapo na baadhi ya watu wanaotoka nchi za magharibi na
hivyo kuwarubuni Watanzania na hivyo kuleta uvunjifu wa amani hapa
nchini.
“Baadhi ya watu wachache ambao wanatoka nchi za magharibi ndio wamekuwa wakituharibia amani yetu hasa pale Mtwara, watu hao wamejaribu kuandika vipeperushi hadi kuviweka rangi ili tu kuwarubuni kwa kuwa wana Mtwara hawawezi kufanya hivyo,” alisema Simba.
Aliwataka wanafunzi hao kutoshabikia mambo yasiyokuwa na msingi na badala yake wasome kwa bidii na wasijihusishe na fujo ambazo hazitawasaidia kitu.
“Ni
lazima mjiamini na kujitambua, msikubali kuyumbishwa na watu
wasiowatakia ninyi mema na kuwaingiza kwenye mambo yatakayowasababisha
kutomaliza elimu yenu na kuvuruga mipango ya maisha ya baadaye,” alisema
Simba.“Baadhi ya watu wachache ambao wanatoka nchi za magharibi ndio wamekuwa wakituharibia amani yetu hasa pale Mtwara, watu hao wamejaribu kuandika vipeperushi hadi kuviweka rangi ili tu kuwarubuni kwa kuwa wana Mtwara hawawezi kufanya hivyo,” alisema Simba.
Aliwataka wanafunzi hao kutoshabikia mambo yasiyokuwa na msingi na badala yake wasome kwa bidii na wasijihusishe na fujo ambazo hazitawasaidia kitu.
Kongamano hilo liliwakutanisha wanafunzi mbalimbali kutoka vyuo vya elimu ya juu Mkoa wa Dodoma, Chuo cha Mipango, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha St John’s, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), pamoja na wanafunzi wa sekondari maarufu kama watoto wa Simba.
No comments:
Post a Comment