Shirika la Afya Duniani,
WHO, linasema inaelekea sana kuwa aina mpya ya virusi vinavouwa, vya
coronavirus, vinaweza kuambukizwa baina ya watu walio karibu sana.
Virusi hivyo ni sawa na vile vya
homa ya SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome) na vinamfanya mgonjwa
kuwa na shida sana ya kuvuta pumzi.
Nchini Ufaransa mwanamume mwengine hivi sasa ni
mahtuti baada ya kuambukizwa na mgonjwa wa mwanzo nchini humo, ambaye
walilazwa chumba kimoja hospitali.
Hadi sasa watu 34 wanajulikana kupata ugonjwa huo duniani tangu mwaka wa 2012, 18 kati yao walikufa Saudi Arabia.
WHO inasema ni muhimu kujulisha watu kuhusu virusi hivyo kwa sababu kuna wasi-wasi mkubwa kuwa vinaweza kusambaa.
Chanzo ni BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment