Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni, Subeti Khamis Faki ameshutumu kitendo cha Baraza la Manispaa Zanzibar kuwanyang’anya bidhaa zao wafanyibishara ndogo ndogo wa maeneo ya Darajani na kugawana mali hiyo bila kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Akitoa malalamiko hayo alidai askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanatumia fursa hiyo ya kujipatia utajiri kwa kuwanyang’anya wafayabishara bidhaa zao kwa mtutu wa bunduki huku wakijifunika nyuso zao na wengine kupaka masinzi hali inayoonyesha kuleta wasiwasi wa uhalali wa uaskari wao.
“Hawa si askari ni majambazi,wezi wa kutumia silaha wanaojinufaisha wao kwa kutumia kivuli cha manispaa kama ni askari wanaotambulika kwa nini wavae ninja, kwa nini watumie mtutu kwa nini wasiwakamate waliofanya makosa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria?alihoji mwakilishi huyo nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi jana.
Kwa siku kadhaa wafanyakazi wa manispaa
wakishirikiana na askari wa vikosi vya ulinzi wamekuwa wakiwafukuza na
kuwapora mali zao wafanyabiashara ndogo ndogo huku wakifyatua risasi
hewani na tukio la mwisho lilitolkea juzi.
Mwakilishi huyo alisema juzi, alishuhudia mwenyewe
tukio hilo kwa askari hao kufyatua risasi na kuanza kukusanya bidhaa za
wafanyabiashara na wale ambao walikusanya bidhaa zao walikuwa wakipigwa
na askari hao
No comments:
Post a Comment