Rais mstaafu wa Mandela Nelson Mandela, bado yuko
hali mahututi ingawa madaktari wanadhibiti hali yake baada ya afya yake
kuzorota mwishoni mwa wiki.
Taarifa kutoka ikulu ya rais zinasema kuwa
Mandela angali yuko chini ya uchunguzi wa madaktari ambao wameweza
kuidhibiti hali yake.
Anaugua maradhi ya mapafu na amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili sasa.
Mapema leo familia yake ilimtembelea
hospitalini, mzee Mandela ambaye anasifika kwa vita alivyopigana dhidi
ya utawala wa wazungu nchini Afrika Kusini.
Amekuwa akiugua ugonjwa wa mapafu mara kwa mara na hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
UJUMBE MBALIMBALI UKIWA UMESAMBAA ENEO LOTE LA NJE YA HOSPITALI |
Rafiki na jamaa wameendelea kukusanyika katika hospitali alikolazwa Mandela mjini Pretoria kumtakia afya njema mzee Mandela.
Mmoja wa waliomtembelea Mandela , mfanyabiashara
Calvin Hugo, aliawachilia huru njiwa weupe, kama heshima yake kwa
Mandela anaeyendelea kuugua hospitalini.
Alisema kitendo chake kilikuwa ishara ya, hatua ya Mandela kuikwamua nchi ya Afrika Kusini kutoka kwa mkoloni.
Baadhi ya jamaa zake wamekusanyika nyumbani kijijini eneo la Qunu, kujadili kile wanachosema ni habari muhimu sana.
WAANDISHI WA HABARI WAMEWEKA KAMBI MDA WOTE TANGU ALAZWE HAPO MZEE MANDELA MTANDAO HUU WA THECHOICE UNAMTAKIA KILA LA HERI APONE HARAKA |
No comments:
Post a Comment