BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limeelezea kupokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii wa tasnia ya muziki
nchini, Albert Mangwea ‘Ngwair’.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA,
Ghonche Materego, baraza limeshtushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na
taarifa ya kifo cha Ngwair, ambaye mchango wake unahitajika sana katika
tasnia ya sanaa, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado
unahitajika katika tasnia hii.
Materego alisema baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na
wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu
wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
“Tunaomba Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya
marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki
kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu,” alisema
Materego.
No comments:
Post a Comment