BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa
msisitizo kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka huu tayari
kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kuanza mara moja na kuzingatia ratiba.
Mkurugenzi wa mawasiliamo wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, alitoa kauli
iyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi
wa habari na kusema kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kujaza fomu za
maombi na kuwa siku ya mwisho ya kupokea maombi hayo ni Juni 30 mwaka
huu.
“Bodi inasisitiza kuanza mchakato wa kuomba mikopo kwa waliomaliza
kidato cha sita na kuzingatia muda uliotolewa kujaza fomu za maombi na
kuziwasilisha kwenye ofisi za bodi,” alisema.
Akizungumzia kuhusu wanafunzi wanaoendelea na masomo, Mwaisobwa
alisema tayari waombaji 62,758 wamekamilisha taratibu za maombi ya
mikopo na kujaza fomu stahiki, tangu utaratibu huo ulipozinduliwa rasmi
Mei Mosi mwaka huu.
“Hadi sasa mchakato kwa waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza na
wanafunzi wanaoendelea na masomo unaendelea vizuri ambapo wengi wamejaza
fomu kwa njia ya mtandao,” alifafanua.
Katika mwaka wa masomo wa 2012/13, bodi hiyo iliwapatia mikopo
waombaji 94,703, ambao wako katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu
ya juu nchini.
No comments:
Post a Comment