Chanzo cha vurugu kuhusu gesi zilizotokea hivi karibuni mkoani
Mtwara, kinaelezwa kuwa ni vuguvugu la kisiasa lililowaingia wananchi
kiasi cha kujenga chuki kubwa dhidi ya Serikali baada ya kupata mahubiri
ya wanasiasa.
Inaelezwa kuwa mzozo huo ulianza rasmi mwaka jana baada ya Serikali kuituma kamati ya kuratibu Maoni ya Sera ya Gesi ambayo ilifika mkoani Mtwara, Novemba 16, mwaka jana kukusanya maoni ya wananchi.
Katika mikutano yake mjini Mtwara, inaelezwa kuwa wananchi wengi hawakukubaliana na wazo la kusafirisha gesi kwenda nje ya Mtwara kwa njia ya bomba.
Hali hiyo ndiyo iliyowafanya viongozi wa vyama vya NCCR-Mageuzi, TLP, UDP, ADC, DP, APPT Maendeleo, Sau na Chauma, kuungana na kuhamasisha wananchi kuhusu suala hilo.
Inaelezwa kuwa hilo lilifanyika Desemba 6, mwaka jana.
Katibu Mkuu wa Muungano huo, Selemani Litope ,alisema mikutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na wananchi ilianza Desemba 12. Mikutano hiyo iliyopewa vibali na Jeshi la Polisi ilifanyika Desemba 12, 16, 19 na 22 na Desemba 27 yalifanyika maandamano makubwa.
“Tuliona kuna malalamiko mengi ya wananchi kuhusu suala gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam, tukaona tuungane ili tufikishe kilio cha wananchi serikalini, kwa sababu tunaamini kwamba, kuisafirisha gesi hiyo ni kuwanyima wananchi fursa ya kufaidika,” alisema Litope.
Alisema katika maandamano yaliyofanyika Desemba
27, Litope alisema walimwandikia Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Mstaafu Joseph
Simbakalia ombi la kutaka ayapokee lakini akakataa na kuwaita kuwa ni
wapuuzi, jambo lililozidisha chuki ya wananchi.
“Kitendo cha mkuu wa mkoa kutuita wapuuzi ,kimeibua chuki kubwa miongoni mwa wananchi, hata hivyo maandamano yetu yalifanikiwa kwa sababu watu wengi walihudhuria na tukafanya mkutano katika Uwanja wa Mashujaa,” alisema.
Hata hivyo, Simbakalia alishaomba radhi kwa kauli yake hiyo Januari mwaka huu kupitia kikao cha majumuisho cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Nani anayetuma vipeperushi na meseji?
Kabla ya vurugu zilizotokea Mei 22 mwaka huu, kulikuwa na vipeperushi na ujumbe wa simu uliosambazwa mjini Mtwara.
Siku hiyo huduma zote za kijamii zisimamishwe ikiwa na maana ya maduka, masoko, daladala, pikipiki n.k ili iwe ujumbe kwa Serikali, maana JK ameamua kutumia nguvu nasi inabidi tupambane naye,” ulisomeka ujumbe huo.
Wakati Jeshi la Polisi likidai kuwakamata watu wawili wanaohusika kusambaza ujumbe wa simu, chanzo cha habari kimeeleza kuwa vipeperushi hivyo huchapishwa mjini Mtwara kwa siri kubwa.
“Hivi vipeperushi vinatengenezwa hapa hapa kwa siri kubwa ila hilo la ujumbe inategemea, mtu anaweza tu kuandika na kuitupa line ya simu. Lengo ni kuhakikisha kuwa mradi wa gesi unakwama kwa njia yoyote,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina.
“Kwa sasa kuna kadi zaidi ya 6,000 ambazo zinapangwa kurudishwa CCM, hatukitaki tena chama hiki Mtwara.Tunafikiria chama kingine cha kutuongoza,” kilisema chanzo hicho mjini Mtwara.
Akizungumza kwa njia ya simu, Makamu Mwenyekiti wa umoja wa vyama hivyo, Abdallah Uledi, alisema wanaotuma vipeperushi na meseji ni wananchi wasiokubaliana na mradi huo.
“Tangu mchakato umeanza Serikali imewahoji viongozi wa siasa, viongozi wa dini, vijana na wazee na wote wameonyesha nia ya kupinga gesi. Hili ni suala la wananchi wote wa Mtwara, siyo wanasiasa peke yake.”
Kwa upande wake, Fatma Sinani wa NCCR-Mageuzi, amesema ujumbe huo ni dalili kuwa wananchi wamehamasika na elimu ya uraia waliyoitoa.
Moja ya waraka uliosambazwa Mei 17, ulisomeka: “Kusini zinduka,
tuungane pamoja, maana dhamira ya Serikali haieleweki kwa mikoa ya
kusini kama mnavyoona.Wote kwa pamoja saa 3.00 asubuhi ya Mei 17, 2013
tusikilize bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni, ili kujua
mustakabali mzima wa gesi yetu na ili kuonyesha kilio/msimamo wetu kwa
Serikali wa kutaka maendeleo kwa mikoa ya kusini.
Siku hiyo huduma zote za kijamii zisimamishwe ikiwa na maana ya maduka, masoko, daladala, pikipiki n.k ili iwe ujumbe kwa Serikali, maana JK ameamua kutumia nguvu nasi inabidi tupambane naye,” ulisomeka ujumbe huo.
Wakati Jeshi la Polisi likidai kuwakamata watu wawili wanaohusika kusambaza ujumbe wa simu, chanzo cha habari kimeeleza kuwa vipeperushi hivyo huchapishwa mjini Mtwara kwa siri kubwa.
“Hivi vipeperushi vinatengenezwa hapa hapa kwa siri kubwa ila hilo la ujumbe inategemea, mtu anaweza tu kuandika na kuitupa line ya simu. Lengo ni kuhakikisha kuwa mradi wa gesi unakwama kwa njia yoyote,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina.
Chanzo hicho kilibainisha kuwepo kwa mkakati wa kuisambaratisha kabisa CCM mkoani Mtwara.
“Kwa sasa kuna kadi zaidi ya 6,000 ambazo zinapangwa kurudishwa CCM, hatukitaki tena chama hiki Mtwara.Tunafikiria chama kingine cha kutuongoza,” kilisema chanzo hicho mjini Mtwara.
Akizungumza kwa njia ya simu, Makamu Mwenyekiti wa umoja wa vyama hivyo, Abdallah Uledi, alisema wanaotuma vipeperushi na meseji ni wananchi wasiokubaliana na mradi huo.
“Siwezi kujua meseji na vipeperushi vinatumwa na
nani, lakini najua kuwa kila namba ya simu imesajiliwa, kwa nini
Serikali isifuatilie?” alihoji Uledi a kuongeza:
“Tangu mchakato umeanza Serikali imewahoji viongozi wa siasa, viongozi wa dini, vijana na wazee na wote wameonyesha nia ya kupinga gesi. Hili ni suala la wananchi wote wa Mtwara, siyo wanasiasa peke yake.”
Aliilaumu Serikali kwa kutotoa elimu ya kutosha kwa wananchi na kwamba matokeo yake ni vurugu.
Kwa upande wake, Fatma Sinani wa NCCR-Mageuzi, amesema ujumbe huo ni dalili kuwa wananchi wamehamasika na elimu ya uraia waliyoitoa.
“Kabla ya kuanzishwa kwa umoja wetu, Serikali
ilituma Kamati ya Nishati na Madini kupata maoni ya wananchi. Kamati
hiyo ndiyo ilituelekeza tutoe elimu kwa wananchi na sisi baada ya
kulitafakari suala hilo tukashtukia mradi huo. Siyo kwamba tumemwaga
sumu kwa wananchi, ila unachokiona sasa ni ukweli uliowaingia wananchi
ndiyo maana hawakubali gesi kusafirishwa.”
Umaskini na ubabe wa Jeshi la Polisi
Kwa upande mwingine, wengi wamekata tamaa kutokana na umaskini wa muda mrefu.
Naye Said Rashid wa Mikindani amelalamikia umaskini: “Hapa hatuna chochote cha kutegemea, samaki tuliokuwa tukivua wametukataza wakisema tunavua kwenye hifadhi ya bahari. Hatuna uwezo wa kununua mitumbwi ya kuvua kina kirefu. Gesi ndiyo hiyo inasafirishwa kwenda Dar es Salaam,” aliongeza.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mfanyabiashara wa Soko Kuu la mjini Mtwara, alisema Serikali ndiyo imeasisi vurugu hizo kwa kuruhusu mikutano na maandamano ya wanasiasa.
“Wanasiasa walipoungana na kuanza kufanya mikutano, walipata vibali vya polisi na hata maandamano yalipofanyika, waliruhusiwa.Leo mambo yamevurugika ndiyo wanaanza kutafuta mchawi.Ndiyo maana kabla ya vurugu za sasa hawakuwahi kukamata mtu,” alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa, Joseph Simbakalia alisema kuwa baada ya maandamano ya Desemba 27, waliwahoji makundi ya watu, lakini hakuna aliyeshikiliwa.
“Tangu vurugu hizo zimeanza Desemba, 2012 tuliwahoji watu kadhaa, ila sina uhakika wangapi,” alisema Simbakalia na kuongeza:
“Hizi ni hujuma na wala hazina uhusiano na suala la gesi. Kama tusingekuwa makini, walitaka kuvunja Daraja la Mikindani, wakataka tena kuvunja Daraja la Mpapura, huko Lindi palikuwa giza tupu, baada ya watu hao kutumia misumeno ya umeme na kukata nguzo za umeme. Walitaka hata kuhujumu Hospitali ya Ligula. Hayo yote yana uhusiano gani na gesi?”
Mlolongo wa matukio.
Maandamano hayo licha ya kutopokelewa na mkuu wa mkoa huo, yalipata kibali cha polisi na kuhudhuriwa na watu wengi.
Madereva wenzake walipoona tukio la mwenzao kupigwa, waliingilia kati mzozo huo na kumtoa mwenzao kwenye kadhia.
Vurugu hizo zilisababisha majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali.
Akizungumza katika mkutano wa majumuisho uliofanyika mjini Mtwara baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, Pinda alisema hakuna tone la gesi ghafi itakayosafirishwa kwa njia ya bomba na kwamba kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajengwa katika Kijiji cha Madimba, mkoani humo ili mabaki yatokanayo na gesi yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda.
Mbali na Waziri Mkuu, Pinda mawaziri wengine waliokwenda Mtwara ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.
Umaskini na ubabe wa Jeshi la Polisi
Licha ya nia njema ya Serikali kutuliza
vurugu kwa majeshi ya ulinzi na usalama, Jeshi la Polisi limeelezwa
kutumia nguvu kubwa kupita kiasi ma hivyo kupoteza imani ya wananchi.
Hali hiyo imejidhihirisha kwa wananchi kuchoma nyumba za polisi na taasisi za Serikali na CCM, ili kuonyesha hisia zao.
Kwa upande mwingine, wengi wamekata tamaa kutokana na umaskini wa muda mrefu.
“Polisi tuliotegemea ndiyo wametutesa, wamechoma
nyumba zetu, wameua tunazika mtu aliyepigwa risasi. Tunanyanyaswa ndani
ya nchi yetu, twende wapi?” alihoji Abdallah Salum wa Mikindani.
Naye Said Rashid wa Mikindani amelalamikia umaskini: “Hapa hatuna chochote cha kutegemea, samaki tuliokuwa tukivua wametukataza wakisema tunavua kwenye hifadhi ya bahari. Hatuna uwezo wa kununua mitumbwi ya kuvua kina kirefu. Gesi ndiyo hiyo inasafirishwa kwenda Dar es Salaam,” aliongeza.
Serikali inakimbia kivuli chake?
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mfanyabiashara wa Soko Kuu la mjini Mtwara, alisema Serikali ndiyo imeasisi vurugu hizo kwa kuruhusu mikutano na maandamano ya wanasiasa.
“Wanasiasa walipoungana na kuanza kufanya mikutano, walipata vibali vya polisi na hata maandamano yalipofanyika, waliruhusiwa.Leo mambo yamevurugika ndiyo wanaanza kutafuta mchawi.Ndiyo maana kabla ya vurugu za sasa hawakuwahi kukamata mtu,” alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa, Joseph Simbakalia alisema kuwa baada ya maandamano ya Desemba 27, waliwahoji makundi ya watu, lakini hakuna aliyeshikiliwa.
“Tangu vurugu hizo zimeanza Desemba, 2012 tuliwahoji watu kadhaa, ila sina uhakika wangapi,” alisema Simbakalia na kuongeza:
“Hizi ni hujuma na wala hazina uhusiano na suala la gesi. Kama tusingekuwa makini, walitaka kuvunja Daraja la Mikindani, wakataka tena kuvunja Daraja la Mpapura, huko Lindi palikuwa giza tupu, baada ya watu hao kutumia misumeno ya umeme na kukata nguzo za umeme. Walitaka hata kuhujumu Hospitali ya Ligula. Hayo yote yana uhusiano gani na gesi?”
Mlolongo wa matukio.
Muungano wa vyama tisa ulipoasisiwa Desemba
6, 2012, umefanya mikutano minne yaani Desemba 12, 16, 19 na 22 kabla
ya kufanya maandamano yaliyoishia Uwanja wa Mashujaa, Desemba 27.
Maandamano hayo licha ya kutopokelewa na mkuu wa mkoa huo, yalipata kibali cha polisi na kuhudhuriwa na watu wengi.
Maandamano hayo yalifuatiwa na vurugu zilizotokea wilayani Masasi Januari 26, 2013.
Chanzo cha vurugu za mkoani Mtwara imeelezwa kuwa
ni askari wanaozunguka mjini na pikipiki maarufu kwa jina la Tigo, baada
ya kumkamata dereva wa pikipiki na kuanza kumpiga.
Madereva wenzake walipoona tukio la mwenzao kupigwa, waliingilia kati mzozo huo na kumtoa mwenzao kwenye kadhia.
Baada ya kumtoa mwenzao, madereva wa bodaboda
waliandamana hadi kituo cha polisi wilayani humo ili kueleza hisia zao
lakini walipofika, polisi walianza kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi
yalioibua hasira za wananchi.
Vurugu hizo zilisababisha majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali.
Kutokana na vurugu hizo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alikwenda mkoani Mtwara kutuliza hali ya mambo.
Akizungumza katika mkutano wa majumuisho uliofanyika mjini Mtwara baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, Pinda alisema hakuna tone la gesi ghafi itakayosafirishwa kwa njia ya bomba na kwamba kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajengwa katika Kijiji cha Madimba, mkoani humo ili mabaki yatokanayo na gesi yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda.
Mbali na Waziri Mkuu, Pinda mawaziri wengine waliokwenda Mtwara ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.
Baada ya hapo mikutano ya uhamasishaji ya muungano wa vyama tisa ikasitishwa.
Hata hivyo, viongozi wa muungano huo, wanasema hawakuridhishwa
na majumuisho hayo kama anavyoeleza Makamu Mwenyekiti wa Mkoa wa Mtwara
wa NCCR-Mageuzi, Mohamed Salim:
“Tulimfuata Waziri Mkuu Pinda huko Dar es Salaam
tukiwa na hoja tatu, kwanza turuhusiwe kuendelea na mikutano ili tutoe
elimu, pili; Mkuu wa Mkoa, Simbakalia aondolewe na tatu, aje Waziri wa
Nishati na Madini ili tuzungumze naye kwa sababu tangu vuguvugu hili
lianze hajawahi kufika huku,” alisema Salim.
Hata hivyo, alisema, Waziri Mkuu atalifikisha
suala la Mkuu wa Mkoa kwa Rais Jakaya Kikwete na kuhusu mikutano
atawasiliana na Waziri Nchimbi na Waziri wa Nishati wa Madini kuhusu
kutembelea Mtwara.
“Hayo yote hayajawahi
kutekelezwa na ndiyo kiini cha vurugu za sasa, kwani wananchi
hawajaridhishwa na ahadi za Serikali,” alisema Salim.
CHANZO CHA HABARI NI WEBSITE YA MWANANCHI
CHANZO CHA HABARI NI WEBSITE YA MWANANCHI
No comments:
Post a Comment