Rehema Chalamila ‘Ray C’.
LEO Michano haitaegemea kwa msanii au staa mmoja. Habari
mbaya ni kwamba baadhi ya wasanii wetu wamejikita kwenye matumizi,
usafirishaji na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Wasanii mna mashabiki wengi. Sibishi katika hilo. Kama mlikuwa
hamjui, mashabiki wanawapenda. Hawapendi kuwaona mkipoteza maisha mkiwa
wadogo kwa sababu ya madawa ya kulevya.
Kama hamjui, madawa ya kulevya au unga au poda au baga kama mnavyoita limekuwa ni janga la kitaifa sasa.
Kama hamjui, madawa ya kulevya au unga au poda au baga kama mnavyoita limekuwa ni janga la kitaifa sasa.
Mkitaka kuamini ninachokisema katizeni mitaa ya Kinondoni-Manyanya,
Dar muone vijana wadogo wanavyovuja udenda wakiwa hawajiwezi kiafya.
Hakika nguvu kazi ya taifa langu inapotea, familia nyingi na taifa
vinaathirika kisa ni starehe inayopatikana katika kubwia unga, uvutaji
bangi, unywaji pombe wa kutupwa, matumizi ya mirungi, shisha na vileo
vingine.
Sawa, kila mtu anahitaji starehe lakini siyo hiyo ambayo kwa sasa mmetumbukia humo.
Kama mlimsikia Prodyuza wa Bongo Records, Paul Mathyasse ‘P-Funky Majani’ alisema kuwa
Kama mlimsikia Prodyuza wa Bongo Records, Paul Mathyasse ‘P-Funky Majani’ alisema kuwa
Albert Mangwea ‘Ngwea’ aliyefariki wiki iliyopita aliingia
kwenye matumizi ya unga kwa sababu ya ‘stress’ tangu mwaka 2006.
Majani alipojaribu kukaa naye kumwambia aache kutumia unga, Ngwea alimwambia kuwa anamtuhumu kwa jambo lisilo la kweli.
Kwa kuwa ni jambo linalohitaji ushahidi sana, Majani alikuwa mpole. Tumwache Ngwea ambaye ameshatangulia mbele ya haki.

Ipo
listi ndefu ya mastaa ambao walishakiri kutumia unga wakaacha. Yumo
Langa Kileo, Aisha Mohamed ‘Madinda’, Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ na
wengine.
Wapo wanaotuhumiwa kwa ishu hizo kama Khaleed Mohamed ‘TID’, Herry Samir ‘Blue’, Seif Shaban ‘Matonya’, Msafiri Sayayi ‘Diouf’, Grayson Semsekwa, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ na wengine japokuwa wamekuwa wakikana.

Stori ya Rehema Chalamila ‘Ray C’ inafahamika. Ilifikia
hatua hadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mrisho Kikwete
akaingilia kati kwenye harakati za kumuokoa kimatibabu baada ya Magazeti
ya Global kutoa picha zake akiwa ‘bwiii’ kwa unga. Hadi leo mambo
hayajatulia kwa upande wa Ray C. Ule muziki wake ulipendwa na mashabiki
wake umebaki historia.
Nimejaribu kuwataja hao wachache lakini ukweli
ni kwamba ishu ya unga ina mapana zaidi. Umewahi kusikia jina la
‘punda?’ Ukisikia msanii anaitwa punda maana yake ni mbebaji wa unga
kusafirisha kupeleka nchi mbalimbali kwa kigezo cha kwenda kufanya shoo.
Ubebaji au usafirishaji huambatana na udhalilishaji ndani yake. Mbebaji humeza kete kadhaa na akifika huko aendako hulazimisha kuzitoa kwa njia ya haja kubwa. Ninyi wasanii mnajua kuwa zoezi hilo hufanyika hadharani. Hebu fikiria unajisaidia mbele za watu huku wao wakihesabu idadi ya kete. Huo siyo udhalilishaji?

Hatari ya kuwa punda ni kwamba ‘mzigo’ unaweza ukapasukia tumboni na kinachofuata ni kifo.
Leo nawabembeleza. Chondechonde wasanii, ninyi ni kioo cha jamii kama mkiungana na kuanza kampeni kubwa ya kupinga unga mtafika mbali. Huu ndiyo wakati wenyewe la sivyo unga utawamaliza. For the love of game!

CHANZO CHA HABARI NA GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment