EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, June 9, 2013

NDOA SI MAIGIZO NI MAISHA KAMILI

 
NAAM, kama ilivyo ada yetu, tumekutana tena kwenye kona yetu. Nina imani kila mmoja hajambo pia nawapa pole wote waliokutwa na matatizo ya misiba na magonjwa. Mungu awalaze pema waliotangulia pia awaponye haraka wote waliokutwa na maradhi.
 
Bila kupoteza muda ningependa nianze mara moja mada yetu ihusuyo ‘thamani ya ndoa’. Naweza kusema nimeandika makala nyingi kuhusu uhusiano, wapo walioelimika kupitia makala hizo na wapo ambao ziliwapitia kulia na kutokea kushoto.
Ndoa ni nini?
Ndoa ni baraka za uhalalisho wa watu wawili wenye jinsia tofauti kuishi pamoja, pia ni muunganiko wa halali wa mwanamke na mwanaume kuwa mwili mmoja. Nina imani mpaka hapo utakuwa umenielewa vizuri zaidi.

Nini thamani ya ndoa kwa mwanadamu?
 Ndoa ni kujitoa katika vitendo vya kuzini yaani kufanya mapenzi pasipo baraka toka kwa Mungu. Ndoa hujenga heshima ya mtu na kumwekea mipaka ya utaratibu wa maisha ambayo humpendeza Mungu. 

Nini nia na madhumuni ya mada hii?
Kutokana na utamaduni wa sasa watu kushindwa kuheshimu ndoa zao kwa kufanya mambo ambayo hayawatofautishi kabla na baada ya kuolewa au kuoa.
Tunashuhudia jinsi wanawake au wanaume wavyotawaliwa na tamaa za kimwili na hutoka nje ya nyumba zao na kuwaacha wenzao wao kama fenicha ndani.

Nini kusudio la kuoa au kuolewa?
Kufunga ndoa ni kuanza maisha safi yampendezayo Mungu, pia kujenga familia nje ya wazazi wako. Mpaka unaamua kuoa lazima utakuwa umeridhika na mpenzi wako na kuwa tayari kuanza safari ya maisha mapya.
Nini kinachotakiwa baada ndoa?
Kwa vile mmeamua kuwa mwili mmoja, basi nyinyi huwa kama viungo vya mwili. Sidhani kama kuna kiungo kitamtegea au kumchukia mwenzake.
Kikiumwa kidole basi mwili mzima huwa taabuni, na katika mapenzi vilevile ni kuwa kitu kimoja au mwili mmoja katika taabu na raha na kuridhika na mwenzako.
 
Hii ni kwa mwanamume kumpenda mkewe na mwanamke kuhuheshimu mumewe. Wanandoa, lao huwa moja, hukaa chini na kujadiliana pamoja kuondoa kero zinazoweza kuweka nyufa ndani yao.
Kuoa ni kufunga mlango wa mabaya yote na kujenga pepo ya duniani. Wana ndoa pendaneni mapenzi ya kweli yenye upendo na huruma. Mke asimuudhi mumewe, vilevile na mume usimuudhi mkewe.
 
Ila kuna watu huingia kwenye ndoa kwa kufuata mkumbo hata hufanya jambo lolote lililo nje ya ndoa bila wasiwasi. Hawa si waoga, wenye kiburi, hawaridhiki na mpenzi mmoja, wametawaliwa na tamaa ya mwili zaidi, waongo na mambo yao mengi yametawaliwa na usiri zaidi.
Hawajutii makosa yao, huamini wapo sahihi kwa kila walifanyalo. Ndoa hizi hazidumu na huvunjika wakati wowote au huwa mateso kwa upande mmoja.
 Aliyeingia katika ndoa kwa dhamira ya kweli ni mpole, mnyenyekevu na mwenye huruma. Huchukia kila lililo baya, ni mwalimu mwema kwa mwenzake na kuwa mbunifu wa kuongeza furaha ndani ya nyumba yao. Ndoa hizi hujaa baraka na amani.
Thamani ya ndoa ni kubwa kuliko unavyofikiria, ndoa si maigizo bali kujitoa kwa ajili ya wenzako na lazima mtafanikiwa.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate