
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema zoezi la utoaji tuzo litaanza saa 3:00 usiku na litapambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali watakaotumbuiza.
“ITV wataonyesha moja kwa moja zoezi zima la utoaji wa tuzo. Tumeamua kuzisogeza kwa wananchi kwa kuandaa ‘skrini’ (viambaza) kubwa ambapo mwaka huu tumeamua kuanza na mikoa mitatu tuone kama zoezi litaenda vizuri ili mwakani tuandae nchi nzima, “alisema Kavishe huku akitaja maeneo ambayo wananchi wataangalia kwenye ‘skrini’ kubwa kuwa ni mabatini (mwanza), CCM Mkoa (Moshi) na Uwanja wa Taifa (Dar es Salaam).
No comments:
Post a Comment