EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, June 4, 2013

WADUDU NI CHAKULA BORA

Repoti mpya ya Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), limetoa taarifa hivi karibuni ikiwahimiza watu duniani kula wadudu kwa wingi kwani ni miongoni mwa vyakula bora, kutokana na kuwa na kiasi kingi cha virutubisho bora vya mwili.
Senene.
Wadudu ni chanzo kikubwa cha protini, mafuta mazuri kiafya, madini na kamba lishe. Aidha, wadudu wameelezwa kuwa ni rafiki wa mazingira na ni rahisi kuwafuga au kuwakamata.

Inakadiriwa na shirika hilo kuwa kiasi cha watu bilioni 2 duniani wanatumia wadudu kama sehemu ya milo yao ya kila siku. Imeshauriwa watu kupendelea kula wadudu kutokana na ukweli kwamba protini inayopatikana kwenye wadudu hao ni bora zaidi  kuliko ile inayopatikana kwenye nyama ya kuku, ng’ombe, nguruwe na samaki.

Mbali ya wadudu kuwa ni chanzo kikuu cha protini na mafuta mazuri kama ya samaki (fish oil), lakini pia ni chanzo kizuri cha madini ya kashiamu (calcium), chuma (iron), seleniamu (selenium), zinki (zinc) na Vitamini B.

Kumbikumbi.
WADUDU WA TANZANIA
Kuna aina zaidi ya elfu tisa ya wadudu wanaoliwa sehemu mbalimbali duniani. Lakini kwa nchini

Tanzania, kuna aina kuu mbili za wadudu ambao wanajulikana na kutumiwa kama sehemu ya kitoweo katika familia nyingi nchini, hasa vijijini.


Aina hizo mbili maarufu nchini Tanzania ni Senene na Kumbikumbi, ambao hupatikana kwa wingi zaidi nyakati za masika sehemu za vijijini. Senene  na Kumbikumbi ni miongoni mwa vyakula vyenye faida nyingi mwilini na ni vitamu pia.

Kutokana na kuwa na faida nyingi za kiafya mwilini, ndiyo maana wamekuwa wakiliwa tangu enzi na enzi na mababu zetu. Ingawa idadi kubwa ya wadudu hao wanaoliwa hupatikana kwa kuwakamata kwenye makazi yao porini, lakini katika siku za hivi karibuni, mifumo ya kisasa ya kuwakamata wadudu hao imebuniwa na hivyo kurahisisha ukusanyaji kwa idadi kubwa na kwa mara moja.

Kwa kuona umuhimu na faida za kiafya zinazoweza kupatikana kwa kula wadudu, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa nchi zote duniani kufuga wadudu hao kwa wingi kibiashara, shirika linaamini nchi nyingi zikitilia mkazo suala hili, zinaweza kupunguza tatizo la njaa kwa kiasi kikubwa na wakati huo huo kuboresha afya za watu wengi.

Bila shaka hii ni habari njema na ya kutia moyo kwa watu ambao tayari wanafuga na kuvuna Senene kibiashara, kama ambavyo tunavyoona wakiuzwa baadhi ya sehemu za mijini. Nitoe wito kwa watu wengine ambao hawajawahi kuonja Senene au Kumbikumbi kufanya hivyo, kwani siyo tu wana faida kiafya mwilini, bali ni watamu sana. (so delicious)!

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate