EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, June 1, 2013

Wengi wafaulu kidato cha sita

Dar es Salaam.
Baraza la Mitihani Nchini (Necta), limetangaza matokeo ya kidato cha sita ambapo asilimia 87.85 wamefaulu huku kundi la shule 20 za mwisho likitawaliwa na shule kongwe nchini na zile za Zanzibar.
Akitangaza matokeo hayo jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde, alisema watahiniwa 50,611 walifanya mtihani huo na kati yao 44,366 sawa na asilimia 87.85, wamefaulu.
Mwaka 2012 wanafunzi waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 46,658 sawa na asilimia 87.65.


Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde akitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2013, kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Watahiniwa wa shule
Dk Msonde alisema kuwa, watahiniwa wa shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya waliofanya mtihani huo.
“Wasichana waliofaulu ni 13,286 sawa na asilimia 95.80 na wavulana 26,956 sawa na asilimia 93.03,” alisema.
Mwaka 2012 watahiniwa 40,775 sawa na asilimia 92.30 walifaulu mtihani huo.
Watahiniwa wa kujitegemea
Alisema kuwa, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo walikuwa ni 7,659 na waliofaulu ni 4,124 sawa na asilimia 53.87.
Ufaulu katika kundi hili umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 5,883 sawa na asilimia 64.96 ya wote waliofanya mitihani hiyo.
Ufaulu kwa madaraja
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, watahiniwa 325 sawa na asilimia 0.76 ya wote waliofanya mtihani huo walipata daraja la kwanza, kati yao wavulana wakiwa ni 188 sawa na asilimia 0.65 na wasichana 137 sawa na asilimia 0.99.

Waliopata daraja la pili ni 5,372 sawa na asilimia 12.54 wavulana wakiwa ni 3,142 sawa na asilimia 10.84 na wasichana 2,230 sawa na asilimia 16.08. Waliopata daraja la tatu ni 30,183 sawa na asilimia 70.45 wavulana wakiwa ni 20,442 sawa na asilimia 70.55 na wasichana 9,741 sawa na asilimia 70.24.
Watahiniwa waliopata daraja la nne 4,362 sawa na asilimia 10.18 ya wote waliofanya mtihani huo huku wavulana wakiwa ni 3,184 sawa na asilimia 10.99 na wasichana 1,178 sawa na asilimia 8.49.
Waliofeli ni 2,604 sawa na asilimia 6.08 wavulana wakiwa 2,021 sawa na asilimia 6.97 na wasichana 583 sawa na asilimia 4.20.

Shule za Zanzibar zaboronga
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, shule kutoka Zanzibar zimefanya vibaya ambapo katika kundi la shule 10 za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 30, saba zinatoka kwenye visiwa hivyo.
Kwa upande wa shule zenye watahiniwa chini ya 30, nne zinatoka Unguja huku shule nyingine kongwe zilizokuwa zikifanya vizuri mwaka huu zimevuta mkia.

Kwa upande wa shule 10 za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 30 ya kwanza kutoka mwisho ni Pemba Islamic College (Pemba), Mazizini (Unguja), Bariadi (Simiyu), Hamamni (Unguja), Dunga (Unguja), Lumumba (Unguja), Osward Mang’ombe (Mara), Green Acres (Dar es Salaam), High View International (Unguja) na Mwanakwerekwe (Unguja).

Shule zilizofanya vizuri zenye watahiniwa chini ya 30, ya kwanza kutoka mwisho ni Mbarali Preparatory (Unguja), Philter Federal (Unguja), St Mary’s (Dar es Salaam, Mzizima (Dar es Salaam), Hijra Seminary (Dodoma), Tweyambe (Kagera), Mpapa (Unguja), Al-Falaah Muslim (Unguja), Presbyterian Seminary (Morogoro) na Nianjema (Morogoro).
 
Shule zilizofanya vizuri
Shule 10 bora katika kundi lenye watahiniwa chini ya 30, ya kwanza ni Palloti Girls (Singida), St. James Seminary, Parane na Sangiti (zote Kilimanjaro), Itamba (Njombe), Masama (Kilimanjaro), Kibara (Mara), St.Luise Mbinga Girls (Ruvuma), St. Peters Seminary (Morogoro) na Peramiho Girls (Ruvuma).

Shule 10 bora katika kundi lenye watahiniwa zaidi ya 30, ya Kwanza ni Mariani Girls (Pwani), Mzumbe (Morogoro), Feza Boys (Dar es Salaam), Iliboru na Kisimiri (zote kutoka Arusha), St Mary’s Mazinde juu (Tanga), Tabora Girls (Tabora), Igowole (Iringa), Kibaha (Pwani) na Kifungilo Girls (Tanga).
Waliofaulu Sayansi

Waliofaulu vizuri kwenye masomo ya sayansi na michepuo yao kwenye mabano ni Erasmi Inyanse kutoka Iliboru (PCM), Maige Majuto kutoka Kisimiri Arusha (PCM), Gasper Mung’ong’o kutoka Feza boys Dar es Salaam (PCM), Gasper Setus kutoka St. James Seminary Kilimanjaro (PCM) na msichana pekee kwenye kundi hili aliyeshika nafasi ya tano ni Lucylight Mallya kutoka Marian Gils Pwani (PCM).
Waliofaulu Biashara
Kundi hili linaongozwa na Eric Robert Mulugo Tusiime Dar es Salaam (ECA), Alicia Filbert kutoka Shule ya Ngaza Mwanza (ECA), Evart Edward, Kibaha Pwani (ECA), Annastazia Renatus Tambaza Dar es Salaam (ECA), Peterson Meena Mbezi Beach Dar es Salaam (ECA).
Lugha na Sayansi ya Jamii
Wa kwanza ni Asia Idd Mti kutoka shule ya Barbro-Johansson ya Dar es Salaam (HGE), Godlove Geofrey Ngowo kutoka shule ya Majengo Kilimanjaro (EGM), Jonson Elimbizi Macha kutoka shule ya Njombe iliyopo Njombe (EGM), Hamisi Joseph Mwita Iliboru Arusha (HGL) na Sia Sand Marian Girls Pwani (EGM).
Matokeo yaliyozuiliwa na kufutwa
Dk Msonde alisema kuwa, Necta imezuia matokeo ya watahiniwa 116 kutoka na sababu mbalimbali, 93 hawakulipa ada ya mtihani, 10 walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya mitihani na 17 walipata matatizo ya kiafya na hawakufanya mtihani hata mmoja.
Alisema pia kuwa, baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa wanne kutokana na kubainika kufanya udanganyifu, kati yao mmoja akiwa ni mtahiniwa wa shule na watatu wa kujitegemea.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate