EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, July 21, 2013

Majambazi wavamia kituo kikuu cha Polisi Mwanza.

Mwanza. 
Majambazi wamevunja ofisi za Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mwanza na kuiba mali mbalimbali vikiwemo vielelezo vya watuhumiwa walio na kesi mahakamani.
Wizi huo wa ajabu ulitokea Julai 18, mwaka huu, ambapo majambazi hao walivunja kituo hicho ambacho ndani yake kuna Ofisi ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC).
 
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zilibaini kuwa majambazi hao walivunja ghala la vielelezo vya washtakiwa, chumba cha ghala la vipuri vya magari ya polisi, zikiwemo ofisi za 
Wapelelezi wa Makosa ya Jinai na Waendesha Mashtaka.

Majambazi hao wanadaiwa kuiba majalada ya kesi, begi lililokuwa na vielelezo vya washtakiwa, kompyuta ndogo mbili (Laptop) za ushahidi na kutoweka.

 Ambapo watu hao ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa waliweza kufanikiwa kuingia ndani ya ofisi hizo za polisi, kwa kuvunja madirisha mawili ya chumba cha ghala la ofisi za Mkaguzi wa Elimu Kanda ya Ziwa ambazo zinapakana na Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati cha Jijini Mwanza, kisha kufanikisha wizi huo.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaeleza kwamba wizo huo ambao ulilenga ofisi ya vielelezo na mashtaka, ulipangwa kwa umakini na kutekelezwa bila ya polisi waliokuwa zamu usiku huo kubaini lolote.
Kwa mujibu wa maelezo wezi hao inadhaniwa ni watu wenye uzoefu na jengo hilo, wakiwa na nia ya kuchukua vielelezo mbalimbali pamoja na mafaili muhimu ya kesi kubwa.

Hili ni tukio lingine kubwa kutokea kwa Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza sambamba na tukio la kuuawa kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, Oktoba 13, mwaka jana ambaye alipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi saa nane usiku wakati akitoka katika kikao cha harusi.

Kauli ya Kamanda Mangu:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Evarist Mangu, amethibitisha kutokea kwa wizi huo na kusema jeshi lake linafanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika, na kusisitiza kuwa kama ni askari wake ama watu toka nje hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Alisema wezi hao waliingilia katika ofisi ya Ukaguzi Elimu Kanda ya Ziwa ambako walivunja madirisha mawili, moja likiwa ni kuingia ndani ya ghala la ofisi za elimu na dirisha lingine la kutokea nje ya ghala hilo, kisha kuvunja dirisha la ndani ya majengo ya polisi na kufanikisha wizi huo.

“Wezi hao walipiga jeki nondo za madirisha hayo, hivyo kung’oka na kuingia ndani kisha kwetu, walianza kuingia katika ghala la polisi la kuhifadhia vifaa vya ofisi vya Jeshi la polisi, lakini inaonekana walikosa cha kuiba, huko walipanda darini na kutokea katika chumba kingine nako hawakuiba, lakini katika chumba cha vielelezo ambako walikuta begi lililokuwa na nguo za vielelezo pamoja na kompyuta ndogo mbili, Lap Top, ambazo walitoweka nazo,” alieleza Kamanda Mangu.

Chumba kingine kinachodaiwa kuvunjwa katika wizi huo ni chumba kinachotunza vipuri vya magari vilivyotumika, ambako Kamanda alidai kuwa hakuna kilichoibwa pamoja na chumba cha vielelezo walikochukua begi la vielelezo.

Mkaguzi wa Elimu Kanda:
Kwa upande wake kaimu Mkaguzi wa Elimu Kanda ya Ziwa, Florencia Vicent, alisema wao hawakugundua wizi huo kutokana na chumba kilichovunjwa kuwa ni ghala, ambacho hakifunguliwi kila mara na kwamba hakikuwa na vitu zaidi ya milango mibovu na maboksi tupu.

“Asubuhi mkaguzi mwenzangu alinieleza kamba wamefika polisi hapa na kudai tumeibiwa hivyo tuliamua kufungua stoo yetu na kuangalia, ambapo tulibaini kuvunjwa kwa madirisha hayo mawili pamoja na dari, lakini inaonekana kama walikuwa wakitafuta njia ya kuingilia na kutoka polisi baada ya wizi,” alieleza mkaguzi huyo.
Alisema ndani ya ghala lao waliweza kukuta suruali mbili mpya moja ikiwa ni aina ya jinsi na nyingine kadeti vikiwa vimetelekezwa ambapo polisi walivitambua kama ni sehemu ya vielelezo vyao na kuondoka navyo.

“Hapa tunaye mlinzi lakini, analinda eneo la ofisi zetu, eneo ambako wezi wameingia lipo chini ya polisi na lina mlango ambao hutumika kupitishia mahabusu, huko wapo polisi, hivyo inaonekana kwetu hakuna kitu kilichoibiwa, mpaka sasa tumefanya ukaguzi wa kina lakini hatuna kitu ambacho kimeibiwa, walengwa katika wizi huo ni polisi na hapa ilikuwa kama njia,” alifafanua kaimu mkaguzi huyo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate