Johannesburg. Kuharibika kwa gari la wagonjwa lililombeba Rais
wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, kulisababisha moyo wa shujaa
huyo kusimama kwa dakika 40.
Hayo yalibainishwa na daktari wa moyo anayemtibu shujaa huyo wa Afrika Kusini, kwamba Juni 8, mwaka huu, wakati akipelekwa hospitali gari lililombeba lilipata hitilafu njiani na kukwama kwa muda.
Daktari huyo wa moyo anayeheshimika nchini Afrika Kusini, (jina linahifadhiwa) alisema jana kuwa gari la wagonjwa lililokuwa likimpeleka Mandela hospitali liliharibika katika njiapanda ya Gauteng na kusababisha wasubiri gari lingine kwa zaidi ya dakika 45.
“Moyo wake ulisimama kabisa tukiwa ndani ya gari, ikatubidi tumfufue kwa mashine (resuscitate),” alithibitisha daktari huyo bingwa.
Ripoti inaeleza kuwa gari hilo la wagonjwa
linalomilikiwa na jeshi, liliharibika wiki tatu zilizopita kati ya
Pretoria na Johanersburg.
Wakati moyo wa Mandela uliposimama, nje kulikuwa na baridi kali kiasi cha nyuzi joto sita tu, hali ambayo inaelezwa kuwa ilichangia kuharibu zaidi mapafu ya Baba wa Taifa la Afrika Kusini.
“Mke wa Mandela, Graca Machel, alikuwa amechanganyikiwa kwa dakika hizo 40, ambazo tulikuwa tukisubiri gari lingine,” kilisema chanzo hicho.
Ingawa msemaji wa Rais Jacob Zuma, Mac Maharaj alisema kuwa madaktari wamethibitisha kuwa Mandela hakupata madhara makubwa kutokana na baridi hiyo, madaktari wengi wameonyesha kupingana naye.
Daktari wa moyo, David Janekelow alisema, kutokana na hali yake, ucheleweshaji wa aina yeyote ile lazima ulisababisha madhara.
“Unahitaji kupata matibabu ya dharura haraka iwezekanavyo. Kama mtu tayari alikuwa anafufuliwa, ucheleweshaji wa kumpeleka hospitali lazima ulete madhara,” alisema Janekelow.
Daktari mwingine wa moyo, Richard Nethonde
alisema, Mandela angekufa pale barabarani wakati wanasubiri gari la
wagonjwa liletwe, imekuwa ni kama bahati hakufa.
Wakati huohuo, wakili wa mjukuu wa Mandela, Mandla Mandela, amesema atafungua mashtaka kwa baadhi ya wanafamilia ya Mandela kwa kuidanganya mahakama kuhusu hali ya shujaa huyo.
Wakili huyo alisema kuwa, wanafamilia hao walipeleka hati hiyo wakiitaka mahakama ichukue uamuzi wa haraka kwani afya ya Mandela ni mbaya, jambo ambalo ni la uzushi.
Wakati hayo yakiendelea, wananchi wengi Afrika Kusini wanaendelea kukusanyika katika viwanja vilivyopo karibu na Hospitali alikolazwa Rais Mandela kumuombea ili apate nafuu mapema.
Wakati huohuo, gazeti la the Sunday Times limeeleza kuwa Graca,
mke wake analala katika chumba kilicho pembeni ya chumba anacholala
Mandela, kwa siku zote, tangu Mandela alazwe.
Wakati huohuo, wakili wa mjukuu wa Mandela, Mandla Mandela, amesema atafungua mashtaka kwa baadhi ya wanafamilia ya Mandela kwa kuidanganya mahakama kuhusu hali ya shujaa huyo.
Wakili huyo, Gary Jansen alisema kuwa wanafamilia
hao walipeleka hati yenye maneno ya uongo mahakamani wakieleza kuwa
Mandela yu mahututi, jambo ambalo limekanushwa na
Rais, Jacob Zuma aliyemtembelea juzi.
Rais, Jacob Zuma aliyemtembelea juzi.
“Tutapeleka malalamiko ambayo yatatokana na hati
ya kiapo iliyopelekwa mahakamani na wanafamilia 15 wa Mandela, kwa ajili
ya kufukua miili ya watoto wa Mandela,” alisema Jansen.
Wakili huyo alisema kuwa, wanafamilia hao walipeleka hati hiyo wakiitaka mahakama ichukue uamuzi wa haraka kwani afya ya Mandela ni mbaya, jambo ambalo ni la uzushi.
“Lazima tufanye uchunguzi wa kutosha kwa sababu mwanasheria wa familia hiyo, ametumia hati ya kiapo vibaya” alisema Jansen.
Wakati hayo yakiendelea, wananchi wengi Afrika Kusini wanaendelea kukusanyika katika viwanja vilivyopo karibu na Hospitali alikolazwa Rais Mandela kumuombea ili apate nafuu mapema.
Habari kutoka ndani ya familia ya Mandela
zinaeleza kuwa huenda mgogoro mkubwa zaidi ukaibuka endapo Mandla
atatimiza azima yake ya kufungua kesi nyingine.
Via Mwananchi.
Via Mwananchi.
No comments:
Post a Comment