Rais Obama akipita kwenye kapeti jekundu huku akiwa na furaha na kucheza nyimbo za wabongo kwenye uwanja wa jijini Dar es salaam wa Mwl. Julius Kambarage mchana wa jana.
Karibu Tanzania....karibu!!!
Ilikuwa ni patashika kwa wacheza ngoma hapa!!! Obama mpaka akaachia Tabasamu
Angalia Rais Obama akicheza nyimbo za hapa kwetu Bongo huku akiwa na furaha kwa mapokezi baada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania siku ya jana hii mchana kwenye muda wa saa nane na dakika 37.

Ulinzi kila kona
Rais na First Lady Obama wakisalimia wananchi wa Tanzanian baada ya kupokewa na Rais Jakaya Kikwete na First Lady Salma
Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Barack Obama wa Marekani akikagua gwaride la heshima wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Baracka Obama akiwapungia wakiangalia vikundi vya ngoma.
Gari alilopanda Rais Obama
Ni furaha hapa baada ya Rais Obama kutua Bongo, hapa anaonekana na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete wakipokewa kwa ngoma
Ni mimi jamani ...tupo pamoja!!Karibu jamani ....jaribu mzee!!! Tunakupenda!!
Mapokezi haya!!! angalia mavazi!!
Rais Obama atakuwepo hapa nchini kuanzia leo Jumatatu tarehe 1 mpaka tarehe 2 kesho kabla ya kuondoka
Hapa ni wakati wapo Africa kusini wakipanda Air Force One Cape Town wakiwaaga wananchi nchini humo kabla ya kuja Bongo Tanzania leo mchana
Rais George W. Bush na mkewe pia wapo hapa nchini Tanzania na pia watajumuika pamoja na Mr Obama Kesho.
Mr Obama alipotembelea jengo la magereza ambapo Nelson Mandela alifungwa kwa miaka kadhaa huko Africa kusini kwenye kisiwa cha Robben Island
No comments:
Post a Comment