EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, July 2, 2013

Rais Obama awasili, aisifu Tanzania.

Dar es Salaam. 
Rais Barack wa Marekani, Obama ametaja vipaumbele vinne vya Marekani kwa Tanzania, ambavyo vinajumuisha miradi mbalimbali ya umeme, miundombinu ya barabara, maji na programu za vijana kwa lengo la kuongeza ajira.
Kiongozi huyo aliwasili Dar es Salaam jana mchana ikiwa ni nchi ya mwisho katika ziara yake barani Afrika ikitanguliwa na Senegal na Afrika Kusini.


Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Rais Obama alisema aliainisha mambo hayo wakati alipozungumza na mwenyeji wake huyo.
Alisema katika mazungumzo hayo, waligusia mradi wa mkubwa wa umeme uitwao Power 

Afrika wenye lengo la kuongeza kiwango cha umeme kinachozalishwa nchini na barani Afrika ili kupata umeme nafuu na wa uhakika utakaochagiza kuongeza uzalishaji na kukuza ajira.

Nchi nyingine za Afrika ambazo zitanufaika na mpango huo ni Kenya, Ghana, Liberia, Nigeria na Ethiopia.

Rais Obama alisema pia wamezungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo, ukuzaji wa demokrasia na utawala bora. Alimzungumzia pia mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hashimu Thabeet anayecheza katika Ligi Kuu ya Marekani (NBA), akiwa na timu ya Oklahoma Thunder ya Marekani, akisema hawakuzungumzia suala lake na kuahidi kufanya hivyo siku nyingine.

Akijibu swali iwapo anaridhishwa na misaada ambayo nchi yake inatoa kwa Tanzania, Rais Obama alisema anafarijika kwa matunda yanayopatikana katika mapambano dhidi ya malaria, barabara mpya zinazojengwa na katika maeneo mbalimbali ya nchi.
“Hatutoi dawa, bali tunajenga miundombinu ya afya, hatutoi chakula, bali kuwezesha nchi kujitosheleza kwa chakula pia tunasisitiza kubadilishwa kwa sheria mbalimbali ili kutoa fursa kwa sekta binafsi kuleta mitaji yao kwa wingi zaidi, lakini jambo la muhimu ni kuijenga Afrika,” alisema.

Kuhusu sekta ya utalii, Rais Obama alisema watatangaza vivutio vya Tanzania, lakini kwa kuwa ameambiwa ujangili ni tatizo, Serikali yake itaisaidia Tanzania kukabiliana na changamoto hiyo.

“Tutatangaza utalii, nimeelezwa ujangili ni tatizo hivyo Marekani itasaidia kupambana na changamoto hiyo na tutaongeza fedha kuhakikisha hali hiyo inatokomea,” alisema.
Akichangia hoja ya misaada ya Marekani, Rais Kikwete alisema Mradi wa Maendeleo ya Changamoto za Milenia (MCC), umekuwa msaada mkubwa kwa Tanzania.

Alisema kupitia MCC, Tanzania imepata msaada wa kujengewa barabara katika maeneo ya vijijini na yale yanayozalisha chakula kwa wingi.
 
Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yamenufaika kwa barabara hizo kuwa ni Namtumbo, Songea, Mbinga, Tunduma, Horohoro, Tanga  na baadhi katika Kisiwa cha Pemba.
Alisema Tanzania pia imenufaika kwa mradi wa maji jijini Dar es Salaam ambao ujenzi wake unaendelea na umeme kwa ajili ya maeneo ya vijijini ambao pia unafadhiliwa na Marekani katika mikoa 10 ya Tanzania.

“Kusema kweli Marekani imefanya makubwa, nikisema inatosha, Mheshimiwa Rais hatasikiliza maombi yangu mengine,” alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisema kutokana na misaada ya Marekani, maambukizo ya Ukimwi yamepungua, vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua na wale wanaozaliwa na wakiwa na VVU wamepungua kwa kiwango kikubwa.

Alisema pia Watanzania wamenufaika na msaada wa vitabu milioni mbili vya sayansi. Alitumia fursa hiyo kuomba idadi nyingine kama hiyo.
“Nimemwambia tunaomba vitabu vingine milioni mbili na yeye akasema niongee na watu wake, lakini nilipowatazama nikaona nyuso zao zinakubaliana na Rais wao,” alisema Kikwete.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliulizwa kuhusu kesi ya Mtanzania aliyeshtakiwa Marekani kwa kumtumikisha binti wa Kitanzania na kushindwa kulipa faini na kusema analifahamu suala hilo, lakini limemalizika kwa wahusika kulipwa.

Alisema binti aliyelalamika alichukuliwa na dada yake kwenda kusomeshwa Marekani, lakini alipofika akatumikishwa kwa kazi za ndani aliwashtaki dada yake na shemeji yake na mahakama ikawatoza faini ya Dola milioni moja za Marekani.

Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kwa wadaiwa kulipa faini hiyo kutokana uwezo wao mdogo, kama ilivyo kwa Watanzania walio wengi, hivyo waliomba faini ipunguzwe na ilipopunguzwa ikalipwa na suala hilo likamalizika.

Aifagilia Tanzania
Akiizungumzia Tanzania, Obama alisema, “Hii ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania, mzee wangu alikuwa Afrika Mashariki na wakati fulani aliishi Tanzania, mke wangu na watoto wangu wamefurahi kufika hapa.”
Alisema alipoingia madarakani Rais wa kwanza kutoka Afrika kukutana naye alikuwa ni Rais Kikwete kwa kuwa Tanzania inaheshimu utawala wa kidemokrasia.

Obama alisema Tanzania imefanya kazi nzuri pamoja na Zanzibar kwa kufanikisha suala la Katiba Mpya kwa ajili ya Tanzania ijayo kwani hiyo ndiyo demokrasia.
Pia aliipongeza Tanzania kuhusu hatua yake katika kulinda amani katika nchi za Jamhuri ya 
Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na Sudan hasa eneo la Darfur. Alisema DRC inaathiriwa na machafuko kutokana na kuwa na maliasili nyingi na kusema Rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila na watu wake wanahitaji kufanya kazi kubwa kuhakikisha amani inakuwapo.
Via MWANANCHI.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate