Rais
wa Marekani, Mhe. Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini leo tarehe
01 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.Katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais
Obama ambaye atafuatana na Mkewe Mama Michelle atapokelewa na Mwenyeji
wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete.Baada ya mapokezi, Mhe. Rais Obama atakwenda Ikulu kwa
mazungumzo rasmi na Rais Mhe. Kikwete.
Aidha, atafanya mkutano na Wafanyabiashara na kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa.Tarehe 2 Julai 2013, Mhe. Rais Obama atatembelea
Mitambo ya kufua Umeme ya Symbion iliyopo Ubungo, Dar es Salaam na
kuzindua rasmi Mpango Maalum wa Maendeleo ya Nishati Barani Afrika
ulioanzishwa na
Marekani
(Power Africa Initiative).Mpango huo utaanza na nchi saba ambazo ni: –
Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Sudan Kusini.Mhe.
Rais Obama anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 02 Julai 2013.IMETOLEWA
NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
30 JUNI, 2013
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
30 JUNI, 2013
Monday, July 1, 2013
-On Monday afternoon, President Obama takes part in a formal arrival ceremony in Dar es Salaam, Tanzania.
-President Obama participates in a bilateral meeting and joint press conference with President Jakaya Kikwete of Tanzania.
-In the evening, President Obama participates in a CEO roundtable and business leaders forum.
-President Obama and President Jakaya Kikwete of Tanzania participate in an official dinner.
Tuesday, July 2, 2013
Tuesday, July 2, 2013
-On Tuesday morning, President Obama takes place in a Consulate meet and greet.
-President Obama visits the Ubungo Power Plant.
Atakapowasili
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na ndege yake
Air Force One, Rais w Maekani, Barack Obama atazindua barabara mpya
upande wa Mashariki wa lango la kuingia Ikulu ambayo inatarajiwa kuitwa
Barack Obama.Baada ya shughuli hiyo atazungumza kwa nyakati tofauti na
wafanyabiashara wa nchi za Afrika na Marekani kwenye hoteli ya Hyatt
Regency, Dar es Salaam.
Amepanga
pia kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani nchini.Baadaye
atahudhuria dhifa ya taifa usiku ambayo imeandaliwa na mwenyeji wake
Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.Kesho ataweka shada la maua
sehemu ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ikiwa ni kumbukumbu ya watu
waliouawa katika shambulizi la kigaidi la bomu mwaka 1998, Dar es
Salaam. Pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Symbion
iliyoko Ubungo.
Obama ametangaza mpango wa kuwajengea uwezo viongozi vijana wa Afrika kwa kuwapa mafunzo ya uongozi katika vyuo vikuu vya Marekani hasa katika masuala ya utawala, biashara na uongozi.
Rais Obama atatoa hotuba kuzungumzia mikakati ya Marekani ya kusaidia Afrika kuzalisha nishati ya umeme.
Michelle
atakuwa na ratiba yake ambapo atapata staftahi na mwenyeji wake, Salma
Kikwete katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), Dar es
Salaam.
Pia
atatembelea sehemu ulikokuwa ubalozi wa Marekani na kisha atashuhudia
onesho la utamaduni la kikundi cha Baba wa Watoto, ambacho kinajumuisha
watoto wa mitaani wenye umri wa kuanzia miaka mitano hadi 18 kwenye
Makumbusho ya Taifa.
Jumanne,
Michelle atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao
pia utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush,
Laura.
Julai
2, Rais Obama atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Symbion Ubungo saa 4
asubuhi na kisha msafara wake utapita Nelson Mandela, Tazara hadi
uwanja wa ndege na kuondoka saa 5.20 asubuhi.
Obama ametangaza mpango wa kuwajengea uwezo viongozi vijana wa Afrika kwa kuwapa mafunzo ya uongozi katika vyuo vikuu vya Marekani hasa katika masuala ya utawala, biashara na uongozi.
Katika
hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Johannesburg juzi jioni, alisema
hatma ya Afrika iko mikononi mwa vijana; hivyo ni lazima wawezeshwe ili
kuliongoza vizuri bara hili.
Alisema
mafunzo hayo yatatolewa chini ya mpango wa ufadhili wa Marekani kwa
viongozi vijana ambao utawajengea uwezo wa kuendesha huduma za
kiserikali ikiwa ni pamoja na biashara na kuhudumia jamii yao.
Kuanzia
mwaka ujao Marekani itatoa mafunzo kwa vijana 500 ambayo yatakuwa ya
wiki sita ambapo idadi hiyo itaongezeka hadi vijana 1,000 kila mwaka.
Watakaofadika
ni vijana wa kati ya umri wa miaka 25 hadi 35 ambao wamekuwa
wakijihusisha na uongozi ndani ya Serikali, sekta binafsi na asasi za
kiraia. Alisema washiriki hao ni lazima waoneshe dhamira yao katika
kuitumikia jamii.
Obama
alisema Afrika ina mwonekano mzuri kwa siku zijazo na kuwataka vijana
wa Afrika kuhakikisha wanatumia uwezo wao katika kutumikia bara lao.
Mpango
wa kuendeleza vijana wa Afrika ujulikanao kama YALI ulizinduliwa mwaka
2010 na Rais Obama ikiwa ni sehemu ya kusaidia maendeleo, kuhamasisha
ujasiriamali na kujenga uwezo wa Afrika kuwa na viongozi bora wa kizazi
kijacho.
No comments:
Post a Comment