EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, July 31, 2013

SERIKALI YATILIANA SAINI NA UINGEREZA UTEKELEZAJI MRADI WA INTERNATIONAL INSPIRATION‏.

 
Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano kuhusu mradi wa International Inspiration awamu ya pili, baina ya Tanzania na Uingereza. Mradi huu umekuwa ukitekelezwa kwa muda wa miaka miwili sasa hapa nchini na unahusisha michezo mashuleni ambapo jumla ya shule 15 zinanufaika na mradi huo.
Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa International Inspiration awamu ya pili leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetiliana saini ya makubaliano na Serikali ya Uingereza katika utekelezaji wa mradi huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto wakiweka saini kwenye mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa International Inspiration leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto wakipeana mikono baada ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa International Inspiration leo jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga  na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto wakionesha kwa waandishi wa habari hati za makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa International Inspiration baada ya kumaliza zoezi la utiaji wa saini leo jijini Dar es Salaam. Mwanafunzi wa  Shule ya Sekondari Azania ambaye pia ni Mwenyekeiti wa Club ya International Inspiration katika shule hiyo Adam Byabato akielezea namna wanavyonufaika na mradi wa International Inspiration kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leornad Thadeo  kiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Henry Lihaya leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa International Inspiration. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga akiwa na baadhi ya wawakilishi wa wanafunzi wanaonufaika na mradi wa International Inspiration wakimskiliza  Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto alipokuwa akifafanua jambo baada ya kumaliza hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mradi huu leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (WHVUM)
---
SERIKALI YATILIANA SAINI NA UINGEREZA UTEKELEZAJI MRADI WA INTERNATIONAL INSPIRATION‏
31/07/2013
Serikali imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wahisani na wadau mbambali ambao wameonyesha nia ya kusaidia kuinua sekta ya michezo hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutiliana saini ya mkataba ya makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa International Inspiration kati ya Serikali ya Tanzania na Uingereza leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Bibi Sihaba amesema kuwa aanaishukuru Serikali ya Uingereza kwa kuchagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ishirini zinazotekeleza mradi huo na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wahisani ambao wamedhamiria kusaidia ukuaji wa michezo Tanzania.

“Ninaishukuru sana Serikali ya Uingereza kwa kuona Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache zinazotekeleza mradi huo,tutaendelea kushirikiana nayi lakini pia nitoa rai kwa wadau wengi kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na yeyote anayetaka kusaidia kukuza sekta ya michezo hapa nchini”. Alsema Bibi Sihaba.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Henry Lihaya amesema kuwa inatia faraja kushuhudia utiaji saini makubaliano ya utekelezaji  wa shughuli za mradi wa International Inspiration (II) ambao ulianza miaka miwili iliyopita.

Ameongeza kuwa walipoanza utekelezaji wa shughuli za mradi huu kumekuwapo mawazo na mipango mingi ya namna bora zaidi ya kuutekeleza mradi huu kwa ufanisi mkubwa ili kuleta mafanikio katika Sekta ya Michezo kwa nchi yetu hasa kwa kuzingatia malengo mazima ya mradi, ambayo ni kuhamasisha vijana kushiriki katika Michezo ili kuboresha maisha yao.

Naye Balozi wa Uingereza hapa nchini Diana Melrose amesema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na  Tanzania katika Nyanja mablimbali ikiwemo sekta ya michezo na kusisitiza kuwa mradi huu umefanikiwa kwa kiasi kikubwa hapa nchini Tanzania.

Mradi wa International Inspiration ulianzishwa mwaka na kamati ya Olympic na Paralympic game ambapo unasimamiwa  na British Council chini ya udhamini wa Uk Sports. Mtekelezaji mkuu wa mradi huu hapa nchini ni Baraza la Michezo la Taifa kwa kushirikiana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, BC, Wadau mbalimbali (TOC, TPC, Shule za sekondari zilizoshirikishwa (15)

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate